Header Ads

MHESHIMIWA ABAMBWA...

DAR ES SALAAM: CHAR/RB/1847/2016 KUJARIBU KUBAKA ni RB ya Kituo cha Polisi Mbagala Charambe jijini hapa  ikimhusu moja kwa moja mheshimiwa Damian Edward Kakuru, mkazi wa Mwandege wilayani Mkuranga, Pwani kufuatia askari wa kituo hicho na ‘makachero’ wa Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kumnasa ndani ya chumba namba 6 kwenye gesti iliyopo Mbagala, Dar akiwa na binti yake (16), jina tunalihifadhi kwa sasa, Wikienda tu linakujuza zaidi. SIKU YA TUKIO Mheshimiwa Kakuru alikumbwa na tukio hilo zito katika kumbukumbu za maisha yake, Septemba 15, mwaka huu akiwa kwenye chumba hicho katika harakati ambazo ziliashiria ni za nia ya kutaka kujaribu kumbaka binti huyo ambaye kisheria yuko chini ya miaka ya kujitambua kwa maamuzi, 18. KWA NINI MHESHIMIWA? Licha ya yale yaliyotokea, mzee Kakuru inadaiwa amekuwa mzee wa Kanisa la Truth Ministry International lakini pia 

 Inatoka Uk. 2 anaheshimika katika jamii ya maeneo anayoishi. Sehemu ya mavazi yake ni zile suti za viongozi huku wengine wanaoonekana kuzivaa sana ni watu wa usalama wa taifa hali inayomfanya asilikwepe jina la mheshimiwa kwa watu wa Mwandege. MWANAYE KIVIPI? Kabla ya kuendelea na tukio hilo, muhimu kufahamu ni kwamba, mzee Kakuru ana wake wanne. Mmoja wa wake zake, anayeishi mkoani, ana mdogo wake wa kike, ndiye mwenye mtoto huyo. Hivyo, alipofika kuishi kwa mzee huyo, maana yake yupo kwa baba yake mkubwa. Na maisha yao nyumbani hapo ni ya mtu na mtoto wake; ‘shikamoo baba, marahaba mwanangu’! SASA TWENDWE PAMOJA Jumba bovu hilo ‘lilimwangukia’ mzee huyo baada ya binti yake kulalamika mara kadhaa kwa watu anaowaamini kuwa, baba yake huyo amekuwa akimshawishi kutenda tukio ambalo yeye anaamini ni la ‘watu wazima’ na wasio na uhusiano wowote. “Binti amedai kuwa kutokana na mazingira hayo kudumu kwa muda mrefu, aliwahi kumshtakia kwa mama yake lakini ilionekana kama mtoto ana uelewa mdogo katika kupokea mambo na kuyatafsiri, lakini pia ilibidi kuwe na kikao cha kifamilia ili kumaliza madai hayo,” kilisema chanzo kimoja. KIKAO CHASHINDWA KUFUA DAFU Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo, licha ya kikao binti huyo alidai baba yake huyo aliendelea kumsumbua hali iliyomsukuma binti, safari hii kuhamishia malalamiko yake kwa walimu katika shule ya sekondari (jina lipo) ambapo binti huyo anasoma na sasa yupo kidato cha nne. WALIMU WAPELEKEWA MALALAMIKO Wikienda lilitajiwa orodha ya walimu ambao, binti huyo alifungua kinywa chake kuwatonya anachokutana nacho kwa baba yake huyo. Walimu hao walitajwa kuwa ni Mapunjo (jina moja, mwalimu mkuu), Adamu Nyema (mwalimu wa malezi), mwalimu Hokororo na mwalimu Said ambao binti huyo alidai wote wanafahamu malalamiko yake. WALIMU NA MAMA MZAZI Chanzo kikazidi kuweka wazi kuwa, baada ya kupokea malalamiko hayo, walimu hao waliwasiliana na mama wa binti aitwaye Goret Kabogwi ambaye anaishi Kamachumu wilayani Muleba, Kagera. “Lakini kinachoonekana ni kwamba, mawasiliano ya walimu na mzazi wa mtoto huyo hayakuzaa matunda kwa kuwa walimu walikuwa wakitaka kumchukua mwanafunzi huyo ili wakaishi naye mpaka atakapomaliza shule arudi kwa mama yake lakini taratibu za kisheria za kuishi na binti huyo zilionekana kuwa ngumu hivyo kumuacha njia panda.” Chanzo. HADI KANISANI Chanzo: “Wakiwa katika kutafuta nini cha kufanya, binti huyo aliendelea kutafuta ufumbuzi mwenyewe ambapo sasa alilipeleka suala hilo kanisani ambako ndiko alikotokea muumini mmoja aliyemuongoza binti huyo
kuwasiliana na OFM na kumhakikishia kwamba, suala lake litakuwa limekoma kama siyo kwisha kabisa! BINTI NA OFM Mungu si Kalimanzila, Septemba 14, mwaka huu, binti alifanikiwa kukutana na OFM uso kwa macho na kusema yote kuhusu mzee huyo huku akirekodiwa kwa sauti na picha kwa ajili ya kuboresha kazi. USHAURI WA OFM Baada ya maelezo yake hayo, OFM walimtaka binti huyo kama ni kweli, kufuata maelekezo kama siyo maagizo. Binti huyo alielekezwa na OFM kumkubalia baba yake huyo ili wanaswe wakiwa gesti, jambo ambalo litaongeza ukweli wa malalamiko yake. Binti: “Sawa, mimi nimewaelewa, lakini sasa nikirudi nyumbani, baba akaniambia tena maneno yake mimi nitawapataje ninyi? Maana sina simu!” OFM: “Sisi tutakupa simu na namba zetu zitakuwemo humo, sawa ee?” Binti: Sawa, nitashukuru sana. Maana nimekuwa sisomi nikaelewa, kisa ni
kusumbuliwa na baba.” OFM: “Usijali binti, yataisha hayo, OFM ni kazi yetu kuhakikisha maadili yanasimama sawasawa na inavyotakiwa.” BINTI NYUMBANI Baada ya kurudi nyumbani, kama kawaida, mzee huyo bila kujua kuwa, OFM wapo kazini, alimwambia binti yake yale maneno. Safari hii, binti alikubali kwa urahisi lakini akaomba eneo la tukio lisiwe nyumbani bali sehemu nyingine yoyote ili kutunza siri. Alipewa maelekezo kuwa, kesho yake, apande daladala kutoka Mwandege hadi Kituo cha Kokoto, Mbagala ambako atakutana na mzee huyo na kutafuta sehemu yenye utulivu kwa ajili ya ‘mazungumzo’ yao. Binti akawasiliana na OFM, akaambiwa good!! SEPTEMBA 15, OFM POLISI Asubuhi ya siku ya tukio, binti huyo aliiambia OFM tayari baba yake ameshamuelekeza eneo la kukutana ambapo OFM nao wakaenda kumjulisha Mkuu wa Upelelezi Polisi Wilaya ya Mbagala (OC-CID), Tobias Walelo na kumueleza mpango mzima. Afande Walelo baada ya kusikiliza kwa umakini maelezo na kuambiwa OFM wanasubiri ushauri wake, alisema amegundua kuna kosa la jinai, aliwataka OFM kwenda Kituo cha Polisi Charambe ambapo ni karibu zaidi na eneo la tukio na
kumtaarifu suala hilo mkuu wa kituo hicho. OFM, ASKARI GESTI Mipango ilisetiwa, maafande wa kituo hicho na OFM waliongozana kwenda gesti kwa maelekezo ya binti huyo kupitia simu ya mkononi ya OFM na kujibanza sehemu kwa siri. Baada ya dakika kadhaa, mzee Kakuru alionekana akiwasili eneo hilo akiwa amevaa suti iliyonyooshwa kwa pasi vizuri. Alimkaribia binti huyo na kumwonesha tabasamu laini kisha wakaanza kukata vichochoro, baba mbele binti nyuma. OFM na polisi wakiwafuata kwa nyuma kimtindo, wawili hao walimaliza vichochoro kadhaa kisha wakatokea kwenye  nyumba ya wageni iliyotulia, walizama ndani kwa pamoja.

POLISI KWA MHUDUMU Polisi walisubiri kwa dakika chache kisha wakaenda kwa mhudumu wa gesti hiyo na kumtaka awaoneshe chumba walichoingia wawili hao. Kwa kutii amri ya jeshi la polisi, mhudumu huyo aliwaonesha chumba namba 6 ambacho alisema hadanganyi!

BINTI ALIVYOJIONGEZA Kwa kuwa katika kuingia ndani ya chumba, binti huyo ndiyo alikuwa nyuma hivyo alitumia nafasi hiyo kuufunga mlango kwa geresha, kitendo kilichowasaidia polisi na OFM walipofika mlangoni kusukuma na kuingia ambapo wawili hao walikutwa nusu utupu!

BABU AJING’ATANG’ATA Baada ya kunaswa laivu, baba huyo aliwatolea macho polisi na kuulizwa kwa nini yuko chumbani na binti huyo ambapo alisema alikuwa na binti yake kwa ajili ya kutatua tatizo fulani lililopo kati yao. “Hapa sisi tumekuja kusuluhisha mgogoro, ninyi mnataka nini? Hebu tuacheni.”

KWA NINI MGOGORO USULUHISHWE GESTI? Mheshimiwa huyo alipoulizwa sababu ya kusuluhishia mgogoro gesti, awali alikaa kimya kisha akasisitiza walikuwa wakitaka kusuluhisha tatizo.

MASHUHUDA WATAKA SHERIA IFANYE KAZI Mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza na OFM waliitaka serikali kusimamia kikamilifu sheria iliyopitishwa kwa kishindo na wabunge mwezi Juni, mwaka huu ya kuwabana wale wote wanaotembea na wanafunzi  na watoto wa kike walio na umri chini ya miaka 18.

MAHOJIANO YALIKUWA HIVI… Kutokana na ufinyu wa nafasi, endelea kufuatilia Magazeti Pendwa ya Global ili kusikia mahojiano kati ya mzee huyo na polisi ndani ya chumba cha gesti. Pia utajua maelezo ya mama mzazi wa binti na walimu wote waliotajwa kupelekewa malalamiko sanjari na hatima ya binti huyo katika masomo na maisha yake nyumbani kwa mzee huyo. Kuangalia video ya tukio hili, tembelea Global TV Online kupitia www. globaltvtz.com.

No comments