Header Ads

Mimba sasa yamtesa Zari

 
 MPENZI wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ anaonekana kuchoka baada ya hivi karibuni picha zake kuvuja zikimuonesha tumbo lake likiwa kubwa.

 
 Zarinah Hassan ‘Zari akiwa katika pozi na marafiki zake.
 Zari ambaye sasa ana ujauzito wa mtoto wa pili wa Diamond unaokadiriwa kuwa wa miezi sita, awali watu hawakuamini kwamb  ni kweli ameamua kubeba mimba nyingine fasta lakini walakini huo sasa unafutika baada ya mimba hiyo kuonekana kukua kila kukicha.

Mmoja wa mawifi wa Zari aliyeomba asitajwe jina alisema kuwa, mimba hiyo sasa inamtesa Zari kwani muda mwingi amekuwa ni mtu wa kukaa ndani na hata kwenye mashughuli siyo kama ilivyokuwa huko nyuma. “Kiukweli ile mimba sasa inamtesa sana Zari, hata Bongo kila akipanga kuja anaahirisha, sijui ni kwa sababu ni mtoto wa kiume? Kikubwa ni kumuombea muda wa kujifungua ufike na ajifungue salama ili furaha ya kaka yetu itimie,” alisema wifi mtu huyo.

No comments