Header Ads

Miss Ilala 2016 Kulamba Mil.1 Ijumaa HiiWashiriki wa Miss Ilala 2016 wakiwa katika picha ya pamoja.


LILE shindano la urembo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa burudani, linatarajiwa kufanyika Ijumaa hii (Septemba 9) ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar ambapo mshindi atakabidhiwa kitita cha Sh. Milioni 1 sambamba na TV kutoka Startimes.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, mratibu wa mashindano hayo, Tickey Kitundu alisema kuwa, mbali na mshindi wa kwanza kulamba Milioni 1, mshindi wa pili atalamba Sh. 700,000, wa tatu Sh. 300,000, wa nne Sh. 200,000 na wa tano Sh. 150,000.

Washindi wengine watapata kifuta jasho cha Sh. 50,000 kila mmoja.

“Tunatarajia Miss Tanzania mwaka huu atoke hapa Ilala hivyo ni fursa kwa wadau wote wa burudani kufika kwa wingi.

“Shindano la mwaka huu litakuwa zuri ambalo halijawahi kutokea kipindi chote cha nyuma, kwa maana urembo ni sanaa kama zilivyo sanaa nyingine na pia ni ajira kwa kina dada,” alisema Tickey.

Usiku huo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa msanii wa Bongo Fleva, Ruby anayetikisa na vibao kibao kama Na Yule, Nivumilie na vingine vingi.


No comments