Header Ads

MKE WA BILIONEA MSUYA AENDELEA KUSOTA RUMANDE


KESI nayomkabili mke wa Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revovatus Muyela ambayo ilikuwa isikilizwe leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar, imeahirishwa, hivyo watuhumiwa hao wataendelea kusota rumande.

Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Magreth Bankika alisema kesi hiyo itasikilizwa Oktoba 10 mwaka huu.

Wiki iliyopita wakili wa washtakiwa, Peter Kibatala aliwasilisha maombi ya wateja wake katika mahakama hiyo, kwa kile alichodai kuwa hati ya mashtaka ilikuwa ina mapungufu kwa kuwa haioneshi kama washitakiwa hao walikuwa wana nia ovu.

Akijibu hoja hiyo ya Kibatala mahakamani hapo, wakili wa serikali, Diana Lukundo alisema hoja zote walizoziwasilisha na upande wa washtakiwa haziko kisheria na kuna aina mbalimbali za kuwasilisha mashtaka.

Baada ya upande huo wa Jamhuri kujibu hoja hizo za upande wa washtakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkazi Mkuu, Bankika, mahakama hiyo ilitarajia kutoa uamuzi wa hoja hiyo leo, hata hivyo, ameahirisha hadi Oktoba 10, mwaka huu.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mnamo Mei 25, mwaka huu maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam, Miriam Mrita na Revocatus Muyela, walimuua kwa kumchinja dada wa bilionea Msuya, Anathe Msuya.No comments