Header Ads

MKUU WA MKOA WA MOROGORO AIPOKEA FURSA



Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Kebwe S Kebwe, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Darasa la Fursa mapema leo kwenye ukumbi wa Midland Msamvu Morogoro.



Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba akiwapa mbinu baadhi ya wakazi wa Morogoro za kujikwamua kwa kutumia Fursa zilizopo Mkoani hapo.



Mkuu wa Chuo cha Mlimani Professional Hassani Ngoma akiwaeleza namana alivyofanikiwa kimaisha wakazi wa Morogoro.



Msanii wa Muziki wa Hip Hop Bongo Nikki wa Pili akiongea jambo kwa wakzi wa Morogoro juu ya kutumia fursa za mkoa huo ili kufanikiwa kimaisha.



Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Steven Kebwe (katikati), akiongea jambo na Ruge baada ya kuwasili ukumbini hapo.



Baadhi ya wafuatiliaji wa semina hiyo wakibadilishana mawazo.




Sehemu ya wakazi wa Borogoro waliojitokeza kujifunza kwenye darasa la kifursa mapema leo.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe akiagana na Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.



MKUU wa mkoa wa Morogoro Mh. Kebwe S. Kebwe, mapema leo alipata muda wa kuwakaribisha na kuwapokea wazungumzaji wa Darasa la Fursa ambalo limekuwa likifanyika kila mkoa ambapo tamasha la Fiesta linafanyika.

Kebwe aliipokea timu nzima ya fursa ndani ya ukumbi wa Midland uliyopo maeneo ya Msamvu mjini Mrogo, ambapo alienda kulifungua darasa hilo na kuwashuhudias baadhi ya wakazi wa mkoa wake walivyojitokeza kusikiliza na kuonyeshwa namna ya kutumia rasilimali za mkoa huko katika kujikwamua.

Akizungumza mara baada ya kuingia katika ukumbi huo Mh, Kebwe alisema kuwa amefurahishwa sana na timu ya Fursa na hasa Clouds Media Group kwa kuwafikishia tamasha la Fiesta ambalo kwake anaamini lina mchango mkubwa sana kwa wananchi wake hasa katika kuongeza kipato na kuwafanya wananchi wake kwa aslilimia kubwa kutumia fursa hiyo kujifunza mambo mengi.

“Nimpongeze sana Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba kwa kutambua umuhimu wetu na kuamua kutuletea tamasha la Fiesta likiwa limeambatana na darasa la Fursa, natambua watu wengi hawaelewi umuhimu wa darasa hili ila kwangu mimi ninajua wananchi wangu watajifunza nini leo kupitia Fursa maana kama ilivyo kauli mbiu yake ni kweli kabisa watu wataongeza thamani kwa kupitia mafunzo haya,” alisema Mh. Kebwe.

No comments