Header Ads

Mo Music adaiwa kutoka na video queen wake

STAA wa Muziki wa Bongo Fleva aliyewahi kubamba na Ngoma ya Basi Nenda, Moshi Katemi ‘Mo Music’ anadaiwa kutoka kimapenzi na video queen wake, Mulki Salum na kwamba wanapika na kupakua. Kwa mujibu wa chanzo, wawili hao awali hawakuwa wakifahamiana ila baada ya kukutana na kufanya Video ya Ngoma ya Ado Ado ambayo imejaa mambo mengi ya chumbani ndipo wakajikuta wakiendeleza kuyafanya yaleyale nje ya kideo.
 
 “Kwa sasa wamekuwa kama kumbikumbi, wanaongozana kila kona na inasemekana wanabanjuka pamoja,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kuunasa ubuyu huo ulioenda shule, Showbiz Xtra ilimtafuta Mo kujibu madai hayo na alipopatikana alifunguka; “Huyo Mulki unayemuongelea nimetokea tu kumzoea sana baada ya ile kazi na ni kweli nipo naye karibu, ila kuhusu kubanjuka naye hapana sijawahi.

” Kwa upande wake modo huyo alipotafutwa alijibu; “Jamani watu kwa kuzua mambo!!! Sawa, hata kama natoka na Mo wao inawa-husu nini, waache kunifuatilia mambo yangu.” Alipobanwa zaidi kuhusu kubanjuka naye aliwaka; “Hakuna kitu kama hicho, Mo ni rafiki wa kawaida kama marafiki zangu wengine.

No comments