Header Ads

Mona ashindana na Zari kuonesha kitumbo

 
Baada ya kuripotiwa na gazeti hili kuwa ni mjamzito, staa wa kitambo wa sinema za Kibongo, Yvonne Cheryl ‘Monalisa’, sasa ameamua kukionesha kitumbo chake huku mashabiki wakidai kuwa anashindana na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni kawaida yake kuonesha tumbo lake. Juzikati Mona alijipiga picha akatupia mtandaoni akidai kuwa ameshiba matunda, hivyo kuibua maneno mengi kwa mashabiki wake waliotaka kujua baba wa mtoto huyo. Kwa mujibu wa wafanyakazi wenzake, Mona ana furaha ya kupata ujauzito huo. Wikienda linamtakia heri katika safari yake ya kuelekea kwenye malezi ya mtoto wa tatu

No comments