Header Ads

Mtangazaji Chanel 10, Cassius Mdami Azikwa leo Moro


cassius-mdami-mazishi-12Gari maalum lililobeba mwili wa marehemu Cassius Mdami likiwa tayari kuelekea makaburini.
cassius-mdami-mazishi-3-001Jeneza la mwili wa marehemu likiwa pembeni ya kaburi kabla ya kushushwa kaburini.
cassius-mdami-mazishi-9-001Jeneza la marehemu likiteremshwa kaburini.
cassius-mdami-mazishi-6-001Mchungaji (aliyeshika biblia pembeni ya msalaba) akiongoza ibada ya mazishi ya marehemu Cassius Mdami.
cassius-mdami-mazishi-2-001Wazazi wa marehemu wakiweka shada la maua juu ya kaburi.
cassius-mdami-mazishi-10-001Mke wa marehemu Rose Msoka (mwenye nguo nyeupe), akisindikizwa na baadhi ya ndugu kuweka shada la maua juu ya kaburi.
cassius-mdami-mazishi-8-001Watoto wa marehemu wakibeba shada la maua tayari kuweka katika kaburi la baba yao mpenzi.
cassius-mdami-mazishi-5-001Baadhi ya wafanyakazi wa Africa Media Group.
 cassius-mdami-mazishi-1-001Mwakilishi wa Africa Media Group, Kibwana Dachi akisoma wasifu wa marehemu mara baada ya maziko hayocassius-mdami-mazishi-7-001
Mmoja wa wanafamilia akisoma wasifu wa marehemu.      cassius-mdami-mazishi-13Marehemu enzi za uhai wake akitoa neno la shukrani mara baada ya kukabidhiwa tuzo za TANAPA, 2014.
cassius-mdami-mazishi-14Washindi wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi aliyekuwa Waziri wa Utalii, Lazaro Nyalandu(wa nne kutoka kushoto waliokaa).
cassius-mdami-mazishi-15Mgeni rasmi, Lazaro Nyalandu akitoa hotuba kwenye ugawaji wa tuzo hizo, 2014.cassius-mdami-mazishi-16Mkurugenzi wa Utalii, Allan Kijazi akitoa hotuba kwenye ugawaji wa tuzo hizo, 2014.
Na Leonard Msigwa/GPL.
Kifo kweli hakina huruma na hakuna ajuaye ni muda gani rohoyake itaacha mwili. Hii ni siri aliyonayo muumba wetu ambaye yeye aijua sekunde, dakika, saa, siku gani ambayo kila mmoja wetu atatangulia mbele za haki.
Naam Septemba 21, 2016 ilikuwa siku ya majonzi kwa wafanyakazi wa Africa Media Group, ndugu, jamaa na marafiki wa Cassius Mdami, ni siku ambayo alihitimisha miaka 44 ya uhai wake hapa duniani tangu alipozaliwa Februari 10,1972.
Kabla ya kukutwa na mauti yake alikuwa mfanyakazi wa Kampuni ya African Media Group akifanya kazi Runinga ya Chanel 10 ambako alikuwa akitangaza Kipindi cha Utalii wa Ndani kilichokuwa kikirushwa kila Alhamisi saa mbili na nusu usiku.
Marehemu alikutwa na mauti hayo baada ya kuugua kwa muda mrefu na alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Mazimbu iliyopo ndani ya Manispaa ya Morogoro.
Leo 24/09/2014 ni tarehe rasmi ambayo ndugu yetu na rafiki yetu Cassius kapumzishwa kwenye makazi yake ya kudumu yaliyopo Kola, Manispaa ya Morogoro, mahali ambako kamwe hatuwezi kuonana naye tena hadi siku ya kiama kama ambavyo maandiko ya vitabu vya kidini yanatueleza.
Ni kweli hatakuwa nasi kimwili lakini mawazo na mchango wake mkubwa kwenye tasnia ya habari nchini utabaki kizazi na kizazi. Atabaki kuwa mwandishi bora na mfano kwa kizazi kijacho kuhusu umuhimu wa kutangaza vivutio vyetu vya utalii vya ndani kwa kina zaidi na kuweza kuiingizia nchi yetu mapato.
Jambo kubwa na muhimu alisaidia kutoa elimu kwa Watanzania wengi ambao hawafahamu chochote kuhusu baadhi ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Marehemu enzi za uhai wake aliwahi kufanya kazi na vituo mbalimbali nchini vikiwemo Kituo cha Redio Tumaini cha jijini Dar es Saalam, Redio Abood ya mjini Morogoro na alijenga jina na kufahamika zaidi alipojiunga na Kituo cha Runinga cha Chanel 10 na kupitia Kipindi cha Utalii wa Ndani aliweza kufahamika na kujipatia umaarufu mkubwa nchini.
Kupitia kipindi hicho marehemu aliwahi kutajwa kuwania tuzo za mwandishi bora wa habari zinazotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) za mwaka 2011. Mwaka 2014 alitajwa na kushinda tuzo za TANAPA katika kipengele cha Mwandishi Bora wa vipindi vya Runinga kupitia chake cha Utalii wa Ndani.
Moja ya vipindi vyake ambavyo vilivuta hisia za Watanzania wengi ni kile kilichoelezea undani na maisha halisi la Kabila la Wahdazabe. Kabila hili ni miongoni mwa makabila yanayokaa na kuishi porini kwa kutegemea mizizi, asali, matunda na wanyama pori na kupitia kipindi hicho aliweza kudadavua undani wa maisha ya kabila hilo, makala hiyo itabaki kama kumbukumbu kwa kizazi na kizazi na ilichangia kuvutia watalii wengi hasa wa ndani waliotaka kujifunza zaidi kuhusu kabila hilo.
Marehemu kaacha mke aitwaye Rose Msoka na watoto watano. Uongozi mzima wa Kampuni ya Global Publishers LTD unaungana na waandishi wa habari kote nchini, ndugu, jamaa, marafiki na familia ya marehemu kumuombea ndugu yetu kwa Mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani milele na milele. AMINA.
PICHA NA MAMREMI, MOROGORO.

No comments