Header Ads

Mwigizaji Aunt Ezekiel Apewa Makavu Baada ya Kudaiwa Kutembea Na Mume wa Shamsa!

TEMA nyongo! Hiyo ndiyo kauli pekee inayoakisi kile alichofunguka Mwigizaji Aunt Ezekiel baada ya kushambuliwa mitandaoni kuwa hana haya kwani kipindi cha nyuma aliwahi kutembea na mume wa staa mwenzake Shamsa Ford, Rashid Said ‘Chid Mapenzi’ lakini siku ya harusi ya shosti yake huyo, alitinga na kusherehekea. 
 
“Jamani Aunt ni mzungu japokuwa alishawahi kuwa na uhusiano na Chid, lakini  anaonekana ni mtu mwenye furaha Aunt acharuka kutembea... na amejumuika vizuri kwenye sherehe ya mwenzake tofauti na watu wengine siku hiyo ya harusi hata hawawezi kwenda,” alinukuliwa mmoja wa waalikwa siku hiyo ya harusi, Septemba 2, mwaka huu. Baada ya harusi hiyo kufanyika na Aunt kuhudhuria mwanzo mwisho akiwa na furaha huku akiimba kwa mbwembwe ule Wimbo wa Hainaga Ushemeji Tunakulaga wa msanii wa Singeli, Amani Fongo ‘Man Fongo’, baadaye mashabiki wa Aunt mtandaoni waliibuka na kumsema kuwa amewaaibisha kwenda kwenye harusi hiyo.

 “Huyu mwenzetu sijui vipi, si bora angetulia nyumbani? Kuna ulazima gani kwenda kwenye sherehe ya  mtu ambaye alikuwa mtu wake?” walihoji baadhi ya mashabiki hao mitandaoni. Baada ya kunyaka maoni mbalimbali yaliyokuwa ‘yakimzodoa’ Aunt, Risasi Jumamosi lilimtafuta mwigizaji huyo na alipopatikana ndipo alipowatemea cheche mashabiki hao waliokuwa wakimponda.

 “Mimi ningeomba kabisa wanikome kwa sababu hawana akili wao wanachojisikia kuropoka wanaropoka na ninawaona kama wapuuzi sana tena wanikome kabisa maana ukinyamaza wanakuona wewe mjinga, niwe nimetembea naye, sijatembea naye wao inawahusu nini? Watu wengine sijui wakoje, waniache bwana na maisha yangu, wao waishi ya kwao wanayoyaona ni sahihi,” alisema Aunt. Kwa upande wa Shamsa, alipoulizwa kama suala la Aunt ‘kubanjuka’ na mumewe amelisikia na amelipokeaje, alisema jambo hilo si la kweli kwani walimwengu wamekuwa wakizungumza mengi baada ya yeye kuolewa lakini kabla ya kuolewa walikuwa kimya. 

“Unajua kabla ya ndoa hakuna nilichokuwa nikikisikia kabisa lakini sasa hivi kila mtu anasema lake hakuna kitu kama hicho na mimi sitaki kuangalia ya nyuma hata siku moja, mimi naanza moja nilipofunga ndoa na mume wangu yaani mbele kwa mbele,” alisema Shamsa

No comments