Header Ads

Mzungu Shoga Anaswa Tena ...Ni yulealiyenaswa akilawitiwa na vijana watatu kwa malipo

DAR ES SALAAM: Sikio la kufa! Si mnamkumbuka yule Mzungu aliyewahi kuandikwa mara mbili na gazeti hili kuhusu skendo yake ya kunaswa akiwa na vijana watatu wa Kibongo kwa madai ya kumlawiti? Kisha akaandikwa ametimka nchini baada ya ishu yake kuandikwa? Sasa amenaswa tena! Wikienda linaripoti kwa kina! Safari hii, Mzungu huyo amenaswa kwenye mtandao mmoja wenye kifupi cha PR akijitangaza huko kuwa, yeye ni shoga na akaanika sifa zake kwa maana ya uwezo wake wa kujiachia na idadi ya wanaume anaomudu kuwa nao kwa wakati mmoja! Lo!

MTANDAO UNA WABONGO KIBAO
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Wikienda lilifanikiwa kunasa mtandao huo ambao cha kushangaza, mbali na kuwepo kwa picha ya Mzungu huyo, pia kuna picha za Wabongo wengine wanaume ambao pia wanajinadi kwa ushoga.

SIFA ZA MZUNGU
Akianika sifa zake kwenye mtandao huo, Mzungu huyo ambaye ilidaiwa ni mwenyeji wa nchi ya Italia aliyeingia nchini Tanzania kufanya kazi kwenye kampuni moja ya ujenzi wa barabara, alisema yeye ni mwanaume mwenye miaka 45. Anajua kuzungumza Kiingereza na Kifaransa. Ana nywele fupi za rangi ya ‘brauni’. Kuhusu uhusiano, yupo singo hivyo anatafuta wanaume weusi, wawe wawili mpaka watatu. Na kwenye mtandao huo aliingia mara ya mwisho Septemba 20, 2016. Kwa sasa Mzungu huyo hayupo nchini.

KILICHOMO KWENYE MTANDAO
Mbali na wanaume hao kuanika picha zao, pia kila mmoja anaeleza sifa zake kulingana na anavyoona. Kuna makundi mawili; wapo mashoga ambao, akitokewa na mwanaume na kumaliza ‘biashara’ yao, yeye shoga ndiye analipa pesa. Hii ndiyo sifa pia ya Mzungu huyo. Lakini wengine, sifa zao ni kulipwa wao baada ya kumaliza kazi. Na pia kundi hili, ukimtaka ukamwita mahali, unamlipia usafiri, iwe ni Bajaj, bodaboda au teksi! 

ALIYEANDIKWA NA IJUMAA NAYE ANASWA
Mbali na Mzungu huyo, kwenye mtandao huo, pia Wikienda lilifanikiwa kumnasa Mbongo anayejulikana kwa jina la Taric aliyewahi kuandikwa na gazeti pacha na hili, Ijumaa la siku ya Ijumaa kwa habari yenye kichwa:

KIGOGO MZITO SERIKALINI SHOGA.
 Katika habati hiyo, kijana Taric alisema kuwa amekuwa shoga tangu kukua kwake na kwamba, kukulia katika mazingira yenye ndugu zake wote wa kike kulichagia kutokana na mazingira yao ya kuoga, kubadili nguo na kujipodoa.     Akasema kutokana na kuwa shoga, amekuwa akitokewa na watu wengi wakimtaka kufanya naye ngono. Alimtaja kigogo mmoja wa serikali kwamba amekuwa na uhusiano naye wa siri kwa muda mrefu.

WIKIENDA LAFANYA KAZI YA UHAKIKI
Mbali na Mzungu na Taric, Wikienda lilifanya kazi ya ziada ili kubaini kama kweli, Wabongo hao ambao wengi ni vijana, wapo nchini au ni picha tu, hivyo, liliwasiliana na mmoja wao moja kwa moja kwenye mtandao huo (online), ikawa hivi: Wikienda: Mambo? Shoga: Poa, niambie. Wikienda: Poa. Inakuwaje, wewe uko wapi? Shoga: Dar, wewe je? Wikienda: Hata mimi, nakupataje? Shoga: Mimi nipo Ubungo River Side, wewe? Tuchati kwenye WhatsApp.

WAKAHAMIA WHATSAPP… Wikienda: Mimi nipo Mwenge.
Shoga: Nitumie picha yako kwanza nikuone.

PICHA! Shoga: Enhe, sasa inakuaje? Wikienda: Wewe masharti yako yakoje? Shoga: Nakuja, baada ya kazi unanipa pesa yangu. Wikienda liliachana naye hapo, lakini tayari ikijulikana kuwa, kweli kuna Wabongo wengi wamo kwenye mtandao huo.

HATARI
Kwa mujibu wa uchunguzi wa Wikienda, wanaume wa Kitanzania ambao wapo kwenye mtandao huo ni wengi kiasi cha kujiuliza nini hatima ya vijana hao?! Mtandao unaonesha kuwa, nchi nzima ina wanaume wanaojishughulisha na ushoga 485. Idadi yao kwenye mabano na mikoa ni kama ifuatavyo: Dar (375), Arusha (56), Dodoma (19), Mbeya (14), Mtwara (2), Mara (1), Tabora (4) na Mwanza 14. Kwa kukujuza tu, Afrika nzima ina mashoga wanaopatikana mitandaoni 53,797.

SERIKALI INAPINGA, LAKINI…
Msimamo wa Serikali ya Tanzania kuhusu ushoga unajulikana kwamba, haikubaliana nao, lakini hali ya mitaani ni tofauti na kukataa kwa serikali kwani kwa sasa, ushoga nchini unazidi kuchipuka kiasi cha kuwa wazi hasa kwenye kumbi za starehe ambapo mashoga hukaa sehemu moja. Ni hatari sana! Kuna maelezo kuwa, kwa sasa ushoga umeingia mpaka kwenye baadhi ya shule za msingi na sekondari nchini, hasa kwenye miji mikuu hali inayoibua maswali kuwa, baada ya miaka kumi ijayo hali itakuaje? Siku za karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliwahi kutoa msimamo wa serikali ya mkoa wake kupinga ushoga na kusema atatumia nguvu kupambana nao.

NENO LA MHARIRI
 Ni vyema kama jamii, wazazi wakafuatilia kwa ukaribu na kujua mienendo ya watoto wao na endapo wakibaini kuwepo kwa viashiria vya vitendo hivyo, wawakanye kabla tatizo halijakuwa kubwa. Tukiungana kwa pamoja kukemea, hakika tutafanikiwa kudhibiti tatizo hili ambalo si tu linapingwa na serikali bali pia linakwenda kinyume na matakwa ya mila na desturi zetu!

No comments