Header Ads

NAY MNANICHUKULIAJE? MIMI SIYO WA KUO

 
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefunguka kuwa jambo la kuoa na kuweka mke ndani atakuwa analisikia kwa wengine tu kwa sababu yeye hana wazo hilo kabisa. Nay alisema, anajua wapo watakaomfikiria tofauti lakini huo ndiyo msimamo wake wa sasa baada kuona jinsi wasanii wenzake waliooa wanavyojuta. “Hivi kwani mnanichukuliaje mimi? Mkinicheki mnaona hii ni sura ya kuoa kweli? Mimi sina mawazo hayo, waache waoe, mimi niponipo sana tu kwa kuwa kuingia huko ni kujipa presha za bure,” alisema Nay

No comments