Header Ads

Ndoa ya Eshe Buheti Yafunjika ...sababu kubwa ni msanii mwenzake!

NDOA ya msanii mahiri wa filamu nchini, Esha Buhet inadaiwa kuvunjika sababu kubwa ikidaiwa kuwa shoga mmoja wa muigizaji huyo kuingilia kati na kujihusisha kimapenzi na mumewe, Risasi Mchanganyiko limedokezwa. 


Chanzo kilicho karibu na familia hiyo kililiambia gazeti hili kuwa familia hiyo imekuwa na mgogoro wa muda mrefu kwa kile kinachodaiwa kuwa mumewe kuwa na tabia ambazo mwanamke huyo alikuwa akizivumilia, lakini baada ya kupata habari za shoga yake kutoka naye kimapenzi, akashindwa kuvumilia. 

“Unajua huyo rafiki yake (jina kapuni) alikuwa mtu wa karibu sana na Esha, tena siku ya kwanza kumpeleka nyumbani kwake, ndipo mumewe akamuona na kuanza kuwasiliana, haieleweki hata mawasiliano walipeana vipi.

 “Sasa hapa katikati Esha alipata safari ya kwenda Uingereza kurekodi filamu, kumbe huku nyuma msichana huyo alihamia kabisa nyumbani hapo na hata msanii huyo alipogundua, msichana huyo hata hakujali chochote, aliendeleza
mapenzi na mume wa mtu kana kwamba hajui huyo mwanaume ana familia yake,” kilisema chanzo hicho. 

Mpashaji wetu anadai msichana huyo amekuwa akiweka picha kwenye akaunti yake ya mitandao ya kijamii akiwa na mwanaume huyo bila hofu yoyote, akimtambulisha kuwa ndiye baba mwenye nyumba. 

Gazeti hili lilimtafuta Esha ili kujua ukweli wa jambo hilo na alipopatikana kupitia simu yake ya mkononi, alisema kwa sasa hayupo katika nafasi nzuri ya kulizungumzia suala hilo. “Naomba uniache kwanza kwa sasa, nitakapokuwa katika ‘mudi’ nitaweza kuanika kila kitu hadharani, naomba tafadhali,” alisema muigizaji huyo. 

Mume wa muigizaji huyo, aliyefahamika kwa jina moja la Nico, ambaye ni kigogo katika taasisi moja ya fedha jijini Dar, alipozungumza na gazeti hili, alisema familia yake iko vizuri, hakuna tatizo. “Mimi sina tatizo kabisa na familia yangu, niko vizuri kabisa, kama kuna mtu anafanya vitu kwenye mitandao ni kwa ajili ya kunichafua na kuniharibia familia yangu,” alisema huku akikataa kutoa ufafanuzi wa kwa nini hachukui hatua za kisheria juu ya mtu huyo anayemchafua mtandaoni.

No comments