Header Ads

Nini Shilole? HIKI NDICHO KIFAA CHA WIZKID


 Shilole akiw katika mapozi tofauti

Utakumbuka hivi karibuni msanii kutoka Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun ‘Wizkid’ alipotua Bongo kwenye shoo ya Fiesta jijini Mwanza, mwanadada Zuwena Mohammed ‘Shilole’ alijinasibu kuwa anapendana na msela huyo.

 Wapo waliojua kwa kauli hiyo kuna uwezekano wawili hao wakaanzisha safari ya kimapenzi. Kama ulikuwa ukiwaza hivyo, futa mawazo hayo kwani Wizkid ana demu wake mkali tu ambaye inaonekana kafa, kaoza kwake.

 Demu huyo ambaye pia ni mwanamuziki anayefahamika kwa jina la Justin Skye, ana umri wa miaka 20 na anatokea nchini Marekani huku akiwa chini ya Lebo ya Roc Nation inayomilikiwa na mkali wa Hip Hop, Jay Z.

 Wiz avujisha Ili kuwaziba midomo wambeya ambao kila kukicha wamekuwa wakimzushia kutoka na mademu mbalimbali, Wizkid kupitia ukurasa wake wa Instagram alitupia picha inayomuonesha akiwa na Justin kisha akaandika: “Kuna swali? Nadhani hakuna swali!” Awali, Wizkid mwenye umri wa miaka 26, anayebamba na ngoma kibao ikiwemo Ojuelegba na Shaba, alikuwa akitoka kimapenzi na mwanamitindo kutoka Nigeria, Tania Omotayo na uhusiano wao ulikuwa wa kuachana na kurudiana.

No comments