• Latest News

  September 17, 2016

  Nuh Mziwanda: Siwezi Kurudiana Na Shilole Ng’o


  Nuh-mziwanda
  Staa wa Bongo Fleva anayetamba na Wimbo wa Jike Shupa, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.
  MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na Wimbo wa Jike Shupa, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amesema kuwa japo kuna tetesi zinaenea mtaani kwamba amerudiana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ suala hilo halina ukweli wowote ndani yake na wala hafikirii kabisa kurudiana na mwanadada huyo.
  Tetesi za Nuh kurudiana na Shilole zilianza kuvuma baada ya kusambaa kwa kipande cha video kilichowaonesha wakipatanishwa wakati wakiwa kwenye safari za Tamasha la Fiesta na watu kujiongeza kuwa wamerudiana.
  nuhumziwanda.png
  Nuh Mziwanda akiwa na mpenzi wake wa zamani Zuwena Mohammed ‘Shilole’.
  “Kilichotokea ni kwamba mimi na Shilole tumeondoa tofauti zetu za kibinadamu ambazo tulikuwa nazo baada ya kuachana.
  Lakini kuhusu kurudiana hahitakuja kutokea hata siku moja na siwezi kurudi nyuma kwenye hili maana nina mpenzi wangu ninayempenda,” alisema Nuh.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Nuh Mziwanda: Siwezi Kurudiana Na Shilole Ng’o Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top