Header Ads

Pam D Adaiwa Kuwachanganya Nay wa Mitego na Roma

MDADA anayefanya poa kwenye gemu la muziki kwa sasa, Pamella Daff a ‘Pam D’ anadaiwa kuwachanganya kimalovee Wanamuziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na Ibrahim Musa ’R.O.M.A’.
 
Madai hayo yameibuka baada ya miezi ya nyuma kidogo mwanadada huyo kunaswa akiwa na Nay kimahaba kwenye gari ambapo walipoulizwa walijing’atang’ata kuonesha kuwa, kuna kitu nyuma ya pazia. Wakati madai hayo yakiendelea kuvuma kuwa Pam D anatoka na Nay licha ya mwanadada huyo kudai yuko singo kwa sasa, juzikati yakaibuka mengine kuwa, staa huyo wa ngoma ya Popolipopo kajiweka kwa R.O.M.A.

 Chanzo ambacho kipo karibu na wasanii hao kilimwaga ubuyu kikisema: “Pam anadai yuko singo lakini yule atakuwa anawachanganya R.O.M.A na Nay, iliwahi kuvuja kuwa Pam D anatoka na Nay lakini sasa hivi yuko karibu sana na R.O.M.A, fuatilieni mtawafuma.”

Kufuatia madai hayo gazeti hili lilizungumza na Pam D ambapo katika majibu yake ilionekana wazi kuna kitu anafi cha ambapo alisema: Pam D: Jamani naomba nisiongee kitu, si unajua R.O.M.A ana mke wake?

 Ijumaa: Kwani kuwa mume wa mtu ndiyo nini? Pam D: Kwa huyo R.O.M.A naomba nisiongee kitu ila Nay ni mtu wangu wa karibu sana na hayo madai kwamba natoka naye siyo mapya. Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta R.O.M.A ili kuzungumzia madai hayo lakini hakuweza kupatikana mara moja, akipatikana atafunguka. Nay naye hakupatikana ila kwenye habari ya kwanza ya wao kunaswa wakifanya yao kwenye gari alikiri kujiweka kwa mwanadada huyo

No comments