Header Ads

PENNY: KUWA SINGO KUNA RAHA YAKE

 
LIYEKUWA Mtangazaji wa Redio Efm ambaye pia ni zilipendwa wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel Mungwilwa ‘Penny’ amefunguka kwamba anajisikia poa sana kuwa singo kwani kuna raha yake.Akipiga stori na Ijumaa kuhusu maisha yake ya kimapenzi kwa sasa, Penny alisema hana mtu na ameamua maisha yake yawe hivyo wakati akijipanga kumtafuta yule wa kuanzisha naye maisha ya ndoa. “Watu hawajajua raha ya kuwa singo, kwanza hufungamani na mtu yeyote na kingine unakwepa maskendo mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii maana huchelewi kuambiwa umebeba mwanaume wa mtu,” alisema Penny.

No comments