• Latest News

  September 30, 2016

  Pluijm: Simba, maneno yenu yote mwisho kesho

  KUELEKEA katika mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi ya Simba, Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amesema imetosha kuhusiana na vita ya maneno inayoendelea kati yao na kinachofuata atawanyamazisha wapinzani kwenye mechi yao hiyo.
   
  Pluijm ameeleza zaidi kuwa wakati mwingine haifai kuongea maneno mengi kuelekea katika mchezo huo kwa kuwa kikosi chake
  kinafahamu nini cha kufanya ili kunyamazisha maneno yote yanayoendelea mitaani kuanzia kwa mashabiki, wapenzi, wadau mpaka viongozi.

  “Huu mchezo umewaweka wengi kwenye presha, sasa sitaki kuongea sana, kuna maneno mengi yameshaongelewa na hii ni kwa kuwa ni mchezo wenye presha kwa sababu ni moja ya utani wa jadi uliopo, sasa kwa upande wetu nadhani hatuhitaji kuongea zaidi ya kufanya kazi hiyo Jumamosi. “Wachezaji wangu wanafahamu mashabiki wanataka nini na nini cha kufanya kuzima hii presha iliyopo kwa mashabiki na wapenzi wengi wa Yanga, kumeshakuwa na maneno mengi lakini sasa ni vizuri kukaa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Pluijm: Simba, maneno yenu yote mwisho kesho Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top