Header Ads

Shamsa Ford aahidi kuwa mke staa wa kuigwa ...leo Ijumaa kufunga ndoa

MSANII mkali kwenye tasnia ya filamu Bongo, Shamsa Ford leo (Ijumaa) anatarajiwa kuyaanza maisha mapya ya ndoa kwa kuolewa na mwanaume anayejulikana kwa jila la
Chidi Mapenzi baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa kipindi kifupi.
 
Akizungumza Shamsa alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumsimamia katika jambo hilo na anaamini akishaingia kwenye maisha hayo ya ndoa, akili yake itatulia na anaahidi kuwa mke mwema.

“Muacheni Mungu aitwe Mungu jamani, amenitendea
mambo makuu sana kwa sababu kuna wengi walidhani nitaaibika tena lakini amenisimamia na aibu hiyo ameikwepesha kwangu, naolewa nipumzike sasa. Nitakuwa mke staa wa kuigwa na watu hawataamini,” alisema Shamsa.

No comments