Header Ads

Shilole, Nuh Mziwanda penzi upyaa!

 
TABORA: Pamoja na kutumia nguvu kubwa kukanusha kurudiana lakini madai mazito yameendelea kuelekezwa kwa mastaa wawili wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ na Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kuwa penzi lao kwa sasa limerejea upyaaa! Habari kutoka kwa chanzo chetu kinachoambatana na wasanii wa Bongo Fleva kwenye ziara za Fiesta mikoani zilieleza kuwa, mara baada ya Nuh kuungana na wasanii hao mkoani Tabora ndipo mambo yakaenda sawa baina ya wawili hao baada ya kupita muda mrefu wa vijembe vya hapa na pale tangu walipomwagana. Chanzo hicho kilinyetisha kuwa, wawili hao, wakiwa kwenye gari la wasanii, walianza kama utani ambapo Shilole alimtaka Nuh kuwa huru kwani yeye yupo kwa ajili yake. 

“Basi kilichofuata yalikuwa ni mabusu ya kufa mtu na kudendeka juu. Kiukweli waliwavutia wengi kwani walionekana kila mmoja alikuwa amemmisi mwenzake. Kuanzia hapo ndipo mambo yakawa freshi, watu wanainjoi uumbaji wa Mungu tu. “Hata baadaye usiku ilisemekana kuwa walilala wote na wala halikuwa jambo la kushangaza kwani walikuwa wamemaliza tofauti zao.

 “Lakini kimbembe kitakuwa kwa Nawali (mpenzi wa Nuh) au Hamadai (mpenzi wa Shilole) maana kuna uwezekano wakaachwa solemba! Itawauma sana aiseee!” kilimalizia kunyetisha chanzo hicho. Baada ya kumwagiwa ubuyu huo, Wikienda lilizungumza na Nuh juu ya sakata hilo ambapo alijitetea kuwa kwa upande wake ana mwanamke wake na kwamba alilazimishwa tu kupatana na Shilole hivyo akaona isiwe ishu bora wayamalize na sasa wako freshi. “Si Unajua uchizi wake (Shilole)? Watu walilazimisha na mimi nikaona yaishe na sasa tupo poa,” alisema Nuh. Kwa upande wake Shilole alifunguka kwa kifupi: “Hahahahaaa…teh… tehee… hakuna kitu kama hicho.”

No comments