Header Ads

Simba Yaipiga Majimaji Nne Kwa Mtungi

Wachezaji wa Simba wakishangilia.

KIKOSI cha Simba, leo kimefanya mauaji ya kutisha mbele ya Majimaji ya Songea baada ya kuichapa mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Simba anayonolewa na Mcameroon, Joseph Omog, ilipata mabao yake kupitia kwa Jamal Mnyate aliyefunga mawili sawa na Shiza Kichuya ambaye naye aliingia nyavuni mara mbili.

Kwa matokeo hayo, Simba imeendelea kukalia usukani kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 16 baada ya kushuka uwanjani mara sita ambapo imefanikiwa kushinda michezo mitano sare mmoja.

Huko Mtwara Azam FC imebanwa mbavu na kuacha alama tatu mbele ya Ndanda baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1. Kesho Yanga inatarajiwa kucheza na Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

No comments