• Latest News

  September 24, 2016

  TANESCO YAWAOMBA RADHI WATEJA WA DAR ES SALAAM WANAOPATA UMEME KUTOKA VITUO VYA KUNDUCHI NA MAKUMBUSHO-KINONDONI KASIKAZINI

  SHIRIKA la Umeme Tanzania ( TANESCO) linapenda kuwataarifu wateja wake wa
  Mkoa wa Dar es Salaam kuwa leo Jumamosi tarehe 24/09/2016 kumetokea hitilafu katika Kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza Umeme cha Ubungo 220kV/ 132kV  na kusababisha kukosekana Umeme kwenye maeneo ya jiji la Dar es Salaam yanayotegemea Vituo vya Kumduchi na Makumbusho.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu jijini mapema leo, tayari hatua za kurekebisha hitilafu hiyo zinaendelea kuchukuliwa ambapo mafundi wa TANESCO wanaendelea na kazi ya kurekebisha hitilafu hiyo na umeme utarejea masaa machache yajayo.

  Taarifa hiyo inawaomba radhi wananchi kutokana na usumbufu wowote utakaojitokeza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TANESCO YAWAOMBA RADHI WATEJA WA DAR ES SALAAM WANAOPATA UMEME KUTOKA VITUO VYA KUNDUCHI NA MAKUMBUSHO-KINONDONI KASIKAZINI Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top