Header Ads

Tibaijuka Aibuka na Tuzo ya Maendeleo ya Bahrain

4

Aliyewahi kuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka, akionesha tuzo aliyoipata mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
 Tibaijuka akionesha cheti alichokipata katika tuzo hizo.

ALIYEWAHI kuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka ameibuka na tuzo ya heshma ya kimataifa ijulikanayo kama ‘Tuzo ya Maendeleo Endelevu ya Mwana Mfalme Khalifa bin Salman Al Khalifa’ aliyokabidhiwa na Waziri Mkuu wa Bahrain, Khalifa bin Salman, ikiwa ni kutambua mchango wake katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Tuzo hiyo aliibuka nayo Septemba 24 mwaka huu katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani ambapo hutolewa kila baada ya miaka miwili na washiriki wakuu huwa ni wale waliowahi kufanya kazi na shirika la Umoja wa Mataifa (UN).


Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Prof. Tibaijuka alisema kuwa viongozi mbalimbali duniani walishiriki kushuhudia tukio hilo huku Tanzania ikisindikizwa na  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga.


No comments