Header Ads

TUKIO LA KUPATWA KWA JUA MBEYA ...PICHA ZOTE ZIPO HAPA JIONEE!

TUKIO la kupatwa kwa jua jana kule Mbeya katika Wilaya ya Mbarali Kata ya Rujewa na wilayani Wanging’ombe, Njombe ndiyo kulikuwa gumzo duniani kote. Wapo ambao wanalisikia tu tukio hilo lakini hawakujua nini hasa kilitokea.

Ijumaa linakupa elimu kidogo Kwa maelezo madogo kupatwa kwa jua ni kitendo cha mwezi (moon) kupita katikati ya jua (sun) na dunia (earth). Kama mnavyojua mwezi na dunia huwa vinalizunguka jua ambalo lenyewe halizunguki. Sasa katika kulizunguka jua ambalo ndiyo chanzo kikubwa sana cha mwanga duniani, pale ambapo mwezi unakaa mbele ya jua lazima kutokee kivuli cha mwezi huo juu ya uso wa dunia ambapo ndiyo eneo hilo huonekana kama usiku japo ni mchana (ilivyokuwa jana Rujewa na Wanging’ombe).

Tukio hilo sasa ndiyo kisayansi linaitwa; Kupatwa kwa Jua (Solar
Eclipse), yaani kivuli cha mwezi juu ya dunia. Lakini hapa ieleweke kwamba, siyo kivuli cha mwezi juu ya dunia yote bali ni sehemu ndogo tu (umbra) ambapo kwa awamu hii ndiyo kwa Tanzania ilikuwa Rujewa na Wanging’ombe japo pia pembezoni ya maeneo hayo palitokea japo giza kidogo (penumbra), halikuwa kali kama kwenye hicho kiini. Kwa hiyo kupatwa kwa jua kunatokea wakati mwezi unafunika jua. Matokeo yake ni kupungua kwa mwanga wa jua hadi kutoonekana tena na kufika kwa giza wakati wa mchana. Muda wa kufunikwa kabisa ni dakika chache tu. Jana ilikuwa dakika tatu tu

No comments