Header Ads

Uchawi wa Simba na Yanga wakamatwa Taifa


VITU vinavyodhaniwa vinatumika kwenye mambo ya kishirikina vimekamatwa juzi usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam lakini upande wa Simba na Yanga umekana kuhusika na ‘mzigo’ huo.
 
Miongoni mwa ‘vifaa’ hivyo ni tunguri, nazi, karatasi zilizofungwa uzi mweusi na kondoo mweusi. Ipo hivi, saa 4:00 siku hiyo makomandoo wa Yanga walishtukia mchezo baada ya kuona mmoja wa walinzi wa uwanja huo ameshika mfuko maarufu kama kiroba na walipomfuata akawaambia amepewa na watu wa Simba.
 
 “Tulipoona hivyo, tukampokonya vile vitu na kuvichoma moto maana kondoo alikuwa mzima ndani ya kiroba, tulimuua na kumfukia nje ya uwanja. Tumezima harakati za Simba,” alisema komandoo mmoja wa Yanga. 
Hata hivyo, mmoja wa makomandoo wa Simba aliyekataa kutajwa jina aliliambia
Championi Jumamosi: “Sisi tulikuwepo uwanjani muda wote na hatukuwa na vitu hivyo, hao ni Yanga wanataka kutuchafua hawana lolote.” Meneja wa Uwanja wa Taifa, Rishe Urio alipotafutwa jana mchana simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa


No comments