Header Ads

Wastara Apata Ubalozi wa Simu za KZG, Atalipwa shilingi Milioni Mia Nne Kwa Mwaka

  Wastara (katikati) akisaini mkataba huo.
Meza kuu wakionyesha aina za simu hizo.


Staa wa filamu Bongo, Wastara Juma amepata shavu la kuwa balozi wa Kampuni ya simu ya mkononi ya KZG ambapo leo amekabidhiwa na kusainishwa mkataba rasmi.
Akizungumza katika tukio la kusaini makubaliano ya kuwa balozi wa kampuni hiyo  lililofanyika katika ukumbi wa De Mag Hotel iliyopo Mwananyamala, Dar,  Wastara alisema amefurahi sana kupata shavu hilo kwani kujituma kwake katika biashara ndiko kulikompatia bahati hiyo.
Aliendelea kusema kwamba atahakikisha anafanya vizuri katika ubalozi huo ambao kwa mwaka unampatia shilingi milioni mia nne kutegemea na jinsi kampuni hiyo inavyouza bidhaa zake hizo kwani imempa heshima kubwa ambayo hakuitarajia.
“Nina furaha sana kuwa balozi wa KZG, hii imetokana na kujituma kwangu kwani ninafanya biashara nami ni mwanamke ambaye ninajitambua na najua ninachokifanya, naishukuru kampuni hii kwa kuniona hivyo, naomba mashabiki zangu waniunge mkono,” alisema Wastara.
Katika tukio hilo pia kampuni hiyo ilimzawadia keki Wastara ikiwa ni zawadi ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake kwani ilikuwa jana, hivyo kutokana na nafasi hiyo wakaona ni vyema wampe zawadi hiyo iliyokuwa imechorwa aina mojawapo ya simu za KZG.

No comments