Header Ads

Wastara, Bond mapenzi upyaa!

STAA wa Filamu za Kibongo, Wastara Juma na meneja wake, Bond Suleiman mapenzi yao yamerejea upya baada ya miezi kadhaa nyuma Wastara kumtosa na kwenda kuolewa na Mbunge wa Jimbo la Donge-Zanzibar, Sadifa Juma. Kurejea kwa penzi la wawili hao kulibainika baada ya hivi karibuni waandishi wa habari hii kufika nyumbani kwa Wastara maeneo ya Magereza Relini jijini Dar na kumkuta Bond akiwa amejaa tele huku wakioneshana mahaba ya
njiwa.
 
 Wastara afunguka  Licha ya kwamba mwanzo zilipovuja taarifa kuwa wamerudiana walikuwa wakitumia nguvu kubwa kukanusha, safari hii walipobambwa hawakuwa na ujanja zaidi ya kuamua kuanika kila kitu kweupe. “Kweli tumeamua kurudi kwenye penzi letu na sikutaka kufunguka mapema kwa sababu siyo kila uhusiano unaufungukia kwani si kila mtu anayependa, nimepitia matatizo mengi na sababu kubwa ni wanadamu hivyo sikuona haja ya kutangaza tena huu uhusiano. “Niliamua kurudi kwa
Bond kwa sababu kiukweli ni mwanaume anayependwa na watoto wangu na anajua mwanamke anataka nini,
mengine ni mipango ya Mungu,” alisema Wastara.

AIZUNGUMZIA NDOA Akizungumzia mipango ya kuoana, Wastara alisema kwa kuwa kila jambo anayepanga ni Mungu ni vyema akaachiwa yeye. BOND NAYE ANENA Bond alipotakiwa k u z u n g u m z i a kurejea upya kwa penzi hilo alisema kwa kifupi: ”Jamani Wazungu wanasema, true love never die… (mapenzi ya kweli kamwe hayawezi kufa).”

No comments