Header Ads

Wema Sepetu kuburuzwa kortini! Kisa kipo hapa

WEMA Isaac Sepetu ‘Madam’ a n a k a b i l i w a na hatari ya kuburuzwa kortini kutokana na kitendo chake cha kutengeneza picha kwa kompyuta (photoshop) akimuonesha akiwa na mtoto anayejulikana kwa jina la Anorah, katika matukio tofauti na kuyaweka kwenye akaunti yake kwenye mitandao ya kijamii bila idhini ya wazazi wake, Risasi Jumamosi limetonywa.
 
 WEMA Isaac Sepetu ‘Madam’.
Kwa mujibu wa chanzo, wazazi wa mtoto huyo ambao siyo Watanzania, walitumia akaunti ya Wema, wakielezea kusikitishwa kwao na tabia hiyo na kueleza kuwa endapo mtoto wao atapatwa na tatizo lolote, basi watamchukulia hatua za kisheria, kwani hawaamini kama vitendo hivyo vinafanyika kwa heri.

 Licha ya Wema mwenyewe, pia baadhi ya mashabiki wake wanaounda kundi liitwalo Team Wema kwa nyakati tofauti, nao wamekuwa wakitengeneza picha za wawili hao na kuzitupia kwenye akaunti ya muigizaji huyo na wakati mwingine, zikimuonesha mtoto huyo akiwa na aliyekuwa mpenzi wake, Idris Sultan. “Unajua mashabiki wa
 


Wema walikuwa wakimpenda huyo mtoto kwa sababu tu amefanana na staa huyo  na walikuwa wakifanya kwa nia nzuri tu, ila wazazi wa mtoto huyo wamechukulia tofauti,” alisema mchangiaji mmoja katika mtandao. Gazeti hili lilimtafuta Wema kwa njia ya simu, ambapo naye alikiri kutokea kwa tukio hilo, akidai picha hizo zilitengenezwa na mashabiki wake kama njia ya kumfariji kwani wanafahamu ana hamu kubwa ya kupata mtoto. 

“Jamani cha busara nilichoona ni kuomba radhi tu, kwa sababu najua kila mtu ana uelewa wake katika  hilo na ninaamini mashabiki wangu walifanya hivyo kwa kunionea huruma  na wakitamani sana  siku moja na mimi niwe na mtoto  wangu, nimewaelewesha wazazi wa Anorah, naamini wataelewa,” alisema Wema. 

 Wema ni mmoja wa mastaa wakubwa wa filamu nchini ambao hawajabarikiwa kupata mtoto licha ya kuwa hivi sasa yuko katika umri unaofaa kuzaa (27) hali ambayo baadhi ya maadui zake wamekuwa wakiitumia kama fimbo ya kumchapia yanapotokea malumbano kati yao.

No comments