• Latest News

  October 31, 2016

  Breaking News: Bondia Thomas Mashali Adaiwa Kuitiwa Kelele za Mwizi, Auawa kwa Kipigo!   Bondia Thomas Mashali maarufu kama ‘Simba Asiyefugika’ ameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kupigwa na watu wasiojulikana baada ya kudaiwa kuitiwa kelele za mwizi, maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam, Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (TPBO), Yassin Abdallah amethibitisha.Thomasi Mashali akiwa katika Pozi uku akiwa na mkanda wake wa Ubingwa wa Taifa unaotambuliwa na TPBO
  Mashali aliyezaliwa kwa jina Christopher Fabian Mashale, inasemekana wakati akinywa pombe, ulizuka ugomvi na mtu mmoja ambaye anadaiwa kupiga kelele kusema Mashali ni mwizi na watu kuanza kumshambulia.
  mashali-na-maugoMabondia Mada Maugo na Thomas Mashali wakitunishiana misuli baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kupambana katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam wakati wa Tamasha la Matumaini Siku ya Sikukuu ya Nanenane (Agosti 8, 2014) lililoandaliwa na Kampuni ya Global Publisher.
  Ndugu zake wanadai kuwa walimkuta akivuja damu nyingi sehemu mbalimbali za mwili wake.
  Taarifa zinadai kuwa alipelekwa katika Hospitali ya Sinza Palestina kabla ya kupelekwa Muhimbili ambako mauti yalimkuta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Breaking News: Bondia Thomas Mashali Adaiwa Kuitiwa Kelele za Mwizi, Auawa kwa Kipigo! Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top