Header Ads

DVJ ALLY B KUWAZAWADIA MASHABIKI WAKE MIXTAPE J’PILI HII

DVJ wa Ukumbi wa Maisha Basement, DVJ Ally B.
Na Mwandishi Wetu
DVJ wa Ukumbi wa Maisha Basement, DVJ Ally B anatarajia kuendelea na utaratibu wake wa kuachia DVD yenye nyimbo mchanganyiko za wasanii mbalimbali (mixtape) iitwayo Fresh From Kitaa.
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi hii ya leo ndani ya ukumbi wa Maisha Basement uliopo maeneo ya Makumbusho jijini Dar, Ally B alisema anatarajia kuizindua mixtape hiyo Jumapili hii ndani ya ukumbi huo hivyo mashabiki wa burudani wafike kwa wingi kuisikiliza kwa pamoja.
“Nimeona nifanye tofauti na ma-DJ wengine wanavyofanya au kuishi kwa mazoea ya kupiga muziki kwenye vituo mbalimbali vya Redio na Televisheni. Sasa mimi nimeamua kuachia mpango huu wa mixtape ambapo kila mwezi nitakuwa nikiachia kwa mashabiki, ya kwanza iliitwa Fresh From Kitaa Volume 1 na safari hii nakuja na Fresh From Kitaa Volume 2,” alisema DVJ Ally B.

Siku hiyo ya uzinduzi, mashabiki 100 wa kwanza watakaowahi kufika, watapewa DVD hiyo bure mlangoni ambapo pia siku hiyo kutakuwa na shoo kali kutoka kwa wasanii mbalimbali walioshirikishwa kwenye mixtape hiyo kama Dogo Janja, Billnass, Barnaba na wengine wengi kwa kiingilio cha shilingi elfu kumi.
DVJ Ally B mbali na kupiga kwenye klabu hiyo, mkali huyo anamiliki chuo cha ma-Dj  kiitwacho Simba Scratch Academy kilichopo Mbalamwezi Beach, Mikocheni jijini Dar na kampuni ya burudani (Ally B Entertainment).

No comments