• Latest News

  October 05, 2016

  VODACOM TANZANIA KUENDELEA NA GULIO LA SIMU-JANJA KWA BEI NAFUU KUPITIA KAMPENI MPYA YA BANDUKA KIJANJA  Kampuni ya simu ya mkononi nchini, Vodacom Tanzania baada ya kufanya gulio mwisho wa wiki iliyopita ambapo simu imara ziliuzwa kwa bei nafuu kuwahi kutokea. 

  Kampuni hiyo inaendelea kuwawezesha Watanzania kumiliki simu imara kwa bei nafuu kwa kuendelea na gulio katika maduka yao 

  “Hatutoacha hadi kila Mtanzania awe ameunganishwa” kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao. 

  Kwa taarifa tulizonazo ni kwamba simu zinazopatikana ni pamoja na Smart 7 na SmartKicka. 

   

  Mteja akifika dukani kwa ajili ya kununua simu mojawapo ya simu hizi anatakiwa kununua kifurushi tu atapatiwa simu ya kijanja na orijino kulingana na kifurushi alichonunua. Mfano, mteja akinunua kifurushi chenye dakika 1,400, SMS 10,000 na 5GB za intaneti atapewa Smart 7 BURE kabisa. 

  Simu zote zitakuwa zimeunganishwa na intaneti ambapo mitandao kama Facebook, Twitter, WhatsApp, Snapchat na Instagram tayari zimeingizwa kwenye simu. 

  Unaweza kutembelea kurasa za Vodacom Tanzania za mitandao ya kijamii kufahamu zaidi au duka la Vodacom lililo karibu yako


   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: VODACOM TANZANIA KUENDELEA NA GULIO LA SIMU-JANJA KWA BEI NAFUU KUPITIA KAMPENI MPYA YA BANDUKA KIJANJA Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top