Header Ads

Kocha Mzambia, George Lwandamina amesaini mkataba wa kuinoa klabu ya Yanga kwa kipindi cha miaka 2

Kwa mujibu wa kituo cha redio E-FM mtangazaji Maulid Kitenge ametangaza kocha wa klabu ya Zesco United, George Lwandamina amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuinoa klabu ya Jangwani Yanga.

Hatua hii imefikiwa baada ya Yanga kutokuwa na matokeo yasiyoridhisha tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi mwaka huu.

Taarifa zaidi zinakujia...

 
Uongozi wa kikosi cha Yanga jana kimemshusha Kocha wa Klabu ya Zesco United, Mzambia, George Lwandamina ili kuweza kumalizana kabla ya kupewa mikoba ya Kocha Pluijm.

Vyanzo mbalimbali kutoka katika Klabu ya Yanga zinasema, Lwandamina alitua nchini jana mchana kwa usiri zaidi, huku uongozi wa Yanga ukimficha kwa kile kilichotajwa kutotaka kuivuruga timu ambayo imerejea kwenye kiwango chake cha kulifukuzia taji la Ligi Kuu, ambapo wamezidiwa na Simba kwa pointi nane huku ikiwa imebakia na mchezo mmoja mkononi.

Mzambia huyo ametinga Bongo kwa lengo la kujadili juu ya maslahi ya kikazi, hali ambayo inatafsiriwa kuwa safari ya Pluijm imewadia.
“Kweli Mzambia huyo amekuja na amekwenda kupokelewa na watu wa kamati ya mashindano lakini alipofikia bado sijapajua, lakini lengo kuu la yeye kuja ni kusikiliza ofa yenyewe,” amesema mmoja wa mabosi ndani ya timu na hakupenda jina lake liandikwe.

Lakini kutokana na usiri huo hakuna ata kiongozi mmoja wa Yanga alikuwa akitaka kuongelea ujio wa Kocha huyo wa Kizambia, huku watu wengine wakisisitiza ujio wa kocha huo.

Tetesi za Yanga kumnyemelea Lwandamina zilikuja wiki kadhaa zilizopita kwa vile Pluijm kutokuwa na maelewana mazuri na baadhi ya wachezaji, hasa baada ya timu hiyo kutetereka kwa kufugwa na Stand bao 1-0, pamoja na sare dhidi ya Ndanda.

Inasemekana kuwa Yanga inataka kulifumua benchi lote la ufundi na kuliunda upya.


No comments