Header Ads

YANGA, AZAM AKUNA MBABE WASHINDWA KUFUNGANA TAIFA LEO


FULL TIME
Mchezo umemalizika, matokeo ni Azam FC 0, Yanga 0.
Dk 94, Mchezo unaweza kumalizika muda wowote kuanzia sasa.
Dk 93, Mchezo umekuwa na kasi ya kawaida, inaonekana pande zote zimeshaona utamalizika kwa suluhu.
Dk 80, Yanga wanafanya mabadiliko, Dante anatoka anaingia Nadir Haroub 'Cannavaro'. Dante aliumia baada ya kuchezewa faulo na kiungo wa Azam FC, Himid Mao.
Dk 78, Azam wanamtoa John Bocco, anaingia Francisco. 
Dk 76, Mwamuzi Israel Nkono anasimamisha mchezo kwa muda, anazungumza na Thomas wa Azam ambaye alionekana kupandwa na hasira na kumfokea mwamuzi wa akiba baada ya kuutoa mpira na kuelekea langoni kwake akidhani ulitakiwa kuelekea upande wa Yanga.
Dk 65, Msuva anaingia na mpira lakini anafanyiwa faulo na kiungo wa Azam, Migi.
Dk 60,Yanga wanapata kona.Inapigwa kona lakini mabeki wa Azam wanaoko.

Dk 50, Azam wanapiga pasi nzuri kuanzia katikati ya uwanja, wanalifikia lango la Yanga lakini mshambuliaji Thomas anashindwa kutumia nafasi anayopata, mabeki wa Yanga wanaokoa. 
Dk 47, Mchezo umeanza kwa kasi ndogo, bado timu zote zinaonekana kusomana.
Kipindi cha pili kimeanza.
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 44, Chirwa anaruka na kuunganisha krosi ya Msuva lakini inakuwa laini kabisa kwa Aishi
Dk 41, Bocco anaachia shuti kali kabisa, lakini Dida anaokoa na kuwa kona
Dk 36 hadi 40, hakuna shambulizi hata moja na mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja
Dk 34, Morris anafanya kazi ya ziada kukoa mpira mbele ya Chirwa na kuwa kona,inapigwa lakini haina faida
 Dk 32, Ya Thomas anaingia vizuri tena na Yanga wanaokoa na kuwa kona, inachongwa na Mudathir, Yanga wanaokoa
Dk 29, krosi ya Ya Thomas inazuiwa na kuwa kona upande wa Yanga, Azam wanaichonga lakini haina makali, Yondania anaondosha 

SUB Dk 27, Mbuyu Twite anaingia kuchukua nafasi ya Juma Abdul aliyeumia
KADI Dk 24, Morris analambwa kadi ya njano baada ya kwenda kumuangusha Chirwa
Dk 23, Mudathir anapiga shuti kali kabisa la mpira wa adhabu, Dida anaokoa vizuri na kuwa kona ya kwanza ya Azam FC
Dk 16, mpira wa adhabu wa Juma Abdul, kichwa safi cha Chirwa lakini Aishi anaonyesha anaweza na kudaka vizuri kabisa

Dk 15, Yanga inapata kona ya tano baada ya shuti la Kamusoko kuokolewa na mabeki wa Azam FC
Dk 13, Azam wanapoteza nafasi nzuri kabisa, krosi nzuri, Ya Thomas anaunganisha lakini kiduchu kabisa inatoka nje ya lango la Yanga
 Dk 10, Azam wanafanya shambulizi kubwa, lakini Yanga wanaokoa na Juma Abdul anachukua mpira na kuanza kazi
KADI Dk 7, Nyoni kalambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Msuva 
Dk 3, Yanga inapata kona ya tatu ndani ya dakika tatu, lakini inakuwa haina madhara tena kwa Azam
Dk 2, Msuva anaingia vizuri kabisa, lakini Azam FC wanaokoa na kuwa kona
Dk 1, Kamusoko anaachia shuti kali lakini kipa Aishi Manula anaokoa na kuwa kona, inachongwa na haina madhara
Dk 1 Mechi imeanza kila upande ukimvizia mwingine

No comments