• Latest News

  October 18, 2016

  Liverpool 0-0 Manchester United


  Pamoja na kuonekana kuwa Liverpool itaibuka na ushindi kwa kuwa iko katika fomu na inacheza nyumbani, mechi hiyo ya Ligi Kuu England imeisha kwa sare ya bila mabao.

  Ilikuwa mechi nzuri, Liverpool wakionyesha kushika vizuri umiliki wa mpira lakini Manchester United wakawa na mashambulizi machache na ya uhakika. 

  Pia Man United, mara kadhaa walitumia ujanja wa kuipoza kasi ya Liverpool huku wakionekana kupoteza muda, jambo ambalo lilikuwa likiwaudhi na hata kuwatoa mchezoni wachezaji wa Liverpool ambao walikuwa wamepania kushinda. 

  Mgawanyiko wa takwimu, kila upande ukichukua kipande fulani, hivyo kuufanya uwe mchezo mzuri na wa kuvutia lakini ambao umemalizika bila ya uhondo wa mabao.

  Liverpool starting XI: 
  Karius, Clyne, Matip, Lovren, Milner, Can, Henderson, Coutinho, Mane, Sturridge (Lallana), Firmino
  Liverpool subs: Grujic, Klavan, Moreno, Lucas, Mignolet, Origi

  Manchester United starting XI: 
  De Gea, Valencia, Bailly, Smalling, Blind, Fellaini, Pogba, Rashford (Rooney), Ander Herrera, Young, Ibrahimovic
  Man Utd subs: Rojo, Mata, Lingard, Carrick, Romero, Shaw

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Liverpool 0-0 Manchester United Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top