Header Ads

Makamuzi Ya Twanga Ndani Ya Toroka UjeBendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Kisima cha Burudani, usiku wa kuamkia leo imefanya makamuzi ya nguvu kwenye Ukumbi wa Toroka Uje, uliopo Tabata Jijini Dar, ikiwa ni maazimisho ya kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere ‘Nyerere Day’.
Kama kawaida kundi zima la bendi hiyo likiongozwa na Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ liliwanogesha mashabiki na kuwafanya kuvamia steji na kujiachia kimadaha.
Bendi hiyo imeufanya ukumbi huo kuwa ukumbi wake wa nyumbani ambapo ‘itakongoli’ kila Ijumaa.

No comments