Header Ads

Malaika: Maprodyuza wananiomba penzi

MWANADADA anayefanya vizuri kwa sasa kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Diana Exavery ‘Malaika’ amefunguka kuwa kutokana na kazi ya sanaa anayoifanya, kila mara amekuwa akikutana na vishawishi vinavyomlazimu wakati mwingine kuhitajika kugawa penzi ili apate pesa au kufanikiwa kimuziki lakini jambo hilo kwake limekuwa gumu kufanya.
 
 Akichonga na Uwazi Showbiz baada ya kubanwa juu ya hilo, Malaika alizidi kutokwa povu na kudai miongoni mwa watu hao wanaomuomba penzi ni maprodyuza lakini yeye huwatolea nje na kuwaambia kuwa hauzi mapenzi na wanatakiwa kuelewa kuwa anajiheshimu.

 “Kiukweli ningekuwa sijali utu wangu mpaka sasa ningekuwa nimekwisha wauzia maprodyuza wengi sana penzi maana wanaonifuata mpaka idadi yao siikumbuki, hata hivyo mimi ni mtu ninayeishi kwa mipaka,” alisema Malaika bila kuwataja maprodyuza hao. 

Hata hivyo, mbali na hilo, Malaika alifungukia juu ya mambo mengine matatu ambayo hawezi kabisa kuyafanya kwa sasa. Jambo la kwanza mrembo huyo anayetamba kwenye gemu na Wimbo wa Rarua Rarua, alisema hawezi kutoka kimapenzi na staa yeyote na anahitaji kuwa na mtu wa kawaida asiyejihusisha na muziki. 

Jambo la pili, hawezi kukubali utu wake kudhalilishwa kwa sababu anataka mafanikio na jambo la mwisho alisema hahitaji kufanya kazi ya kiwango cha chini, kutoka alipo anahitaji kusogea mbele ili aweze kuupeleka muziki wakwe kwenye anga za kimataifa.

No comments