Header Ads

Mbao FC inamdai Waziri wa Magufuli Sh 600,000

TIMU ya Mbao FC ya jijini Mwanza, jana ilishuka uwanjani kukipiga dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kupata ushindi pamoja na kuongeza pato lao kutoka kwa waziri ambaye pia ni mbunge.
 
Mbao FC inayoshiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza iliahidiwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula
kuwa atanunua kila bao watakalofunga kwenye ligi hiyo kwa shilingi 50,000.

Katibu Mkuu wa Mbao FC, Richard Athanas, ameliambia Championi Ijumaa kuwa kabla ya mchezo wa jana, ahadi yao kutoka kwa kiongozi huyo aliye chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ilikuwa imeļ¬ ka shilingi 600,000 kutokana na mabao waliyofunga.

CHANZO: CHAMPIONI

No comments