• Latest News

  October 01, 2016

  Msuva: Napitia kulekule kwa Tshabalala

  BEKI wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’, maarufu kama Tshabalala, amesema ataweka ulinzi mkali kwa mawinga wa Yanga wasipite kwake leo, lakini Simon Msuva amesema atapita hukohuko katika upande wake.
   
   Yanga na Simba zinacheza leo mchezo namba 43 wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo tayari Tshabalala
  ameshapiga mkwara kwamba hataruhusu mtu kupita upande wake. Kwa upande wake, Msuva ambaye ni winga anayemudu kucheza upande wa kulia, alisema: “Nimemsikia Tshabalala akitamba kuwa hatuogopi, mimi namwambia tutaonana uwanjani.

  “Ninaamini nitafanya kazi yangu kama kawaida na nitapitia hukohuko alipo yeye (Tshabalala) kwani nimefanya mazoezi makali kujiandaa na mchezo huu.” Msuva alisema hapendi kumzungumzia mchezaji wa timu pinzani, lakini amelazimika kutoa kauli hiyo kwa Tshabalala ili kuwatoa hofu mashabiki wa Yanga wanaodhani anaweza kuzuiwa na beki huyo.

  “Tshabalala yeye kama anaongea hivyo, mwacheni tu, lakini kikubwa anatakiwa kutambua kuwa soka linachezwa uwanjani na siyo mdomoni,” alisema Msuva ambaye hadi sasa ana bao moja katika ligi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Msuva: Napitia kulekule kwa Tshabalala Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top