Header Ads

Mwamuzi akiharibu leo imekula kwake

KATIKA mchezo wa leo wa Simba na Yanga, mwamuzi wa kati ni Maartin Saanya mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), sasa akichemsha tu imekula kwake.

 Saanya mkazi wa Morogoro, atasaidiwa na Samuel Mpenzu wa Arusha na Ferdinand Chacha wa Mara na Herry Kafir wa Dar es Salaam atakuwa mwamuzi wa akiba. 

Sasa Saanya amewekewa mtego na kama akichemsha katika kazi yake leo, basi atapunguziwa mechi za kuchezesha za Ligi Kuu Bara msimu huu katika mzunguko wa pili. 


Huko nyuma ambako waamuzi walikuwa wakila shavu la kuchezesha mechi nyingi, mpaka sita kwa mzunguko mmoja, safari hii mambo yamebadilika. 

Kama leo Saanya akichemsha na kamisaa akaandika uozo wake, mwamuzi huyo atazikosa mechi za mzunguko ujao. Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa Soka Tanzania (Frat), Nassor Mwalim, alisema: “Hatujapanga waamuzi wa mzunguko wa pili mpaka tutakapofanya tathmini za waamuzi katika mzunguko huu wa kwanza.

No comments