Header Ads

Nicki Minaj Adaiwa Kuachana Rasmi na Meek

Madai ya Nicki Minaj kumwagana na Meek Mill yalianza kuvuma tangu Agosti, mwaka huu lakini juzikati yalitokea mazingira ya kudhihirisha ni kweli penzi kati ya wawili hao halipo tena.
Kudhihirika huko kumekuja baada ya wadau wa Lebo ya Muziki ya Tidal akiwemo Beyonce na mumewe Jay Z na TI kujumuika pamoja kwenye chakula cha usiku ambapo licha ya Meek kuwa mmoja wao, hakuonekana na badala yake Nicki alifika peke yake.
22-nicki-minaj-meek-mill-w529-h352
Mbali na hilo inaelezwa kuwa, kuna matukio kadhaa ya hivi karibuni ambayo iliratajiwa Nicki aonekane akiwa na Meek lakini haikuwa hivyo, kitu kinachowafanya wengi kuamini kuwa, penzi la wawili hao limevunjika rasmi.

No comments