Header Ads

Picha za Mechi Ya Yanga na Azam, yamalizika kwa sare ya bila kufungana jana

AZAM ikiwa mwenyeji kwenye Uwanja wa Uhuru mbele ya Yanga imeshindwa kubakiza alama tatu baada ya mchezo wao kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mchezo huo ambao ulijaa ubabe mwingi, ulishuhudia mwamuzi Israel Nkongo akitoa kadi za njano tano huku nne zikienda kwa Azam na moja kwa Yanga.

Katika mchezo huo washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Donald Ngoma wa Yanga na wale wa Azam waliokuwa chini ya nahodha John Bocco walikosa nafasi nyingi za kufunga mabao lakini uwezo wa makipa wa timu zote uliwafanya washindwe kutikisa nyavu zao.

Takwimu zinaonyesha Azam walicheza faulo 17 na Yanga 10, mashuti yaliyopigwa na Azam na kulenga lango yalikuwa matano kwa Azam na Yanga sita.No comments