• Latest News

  October 10, 2016

  Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Mhandisi James Mitayakingi Kilaba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

  Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi James Mitayakingi Kilaba umeanza jana Jumamosi tarehe 08 Oktoba, 2016.

  Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi James Mitayakingi Kilaba alikuwa akikaimu nafasi hiyo, baada ya uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba kutenguliwa.

  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam

  09 Oktoba, 2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top