• Latest News

  October 21, 2016

  SAMATTA ATOKEA BENCHI NA KUISAIDIA GENK KUITWANGA BILBAO MABAO 2-0 EUROPA CUP


  KRC Genk imeonyesha si timu ya mchezo baada ya kuitwanga Athletic Bilbao ya Hispania kwa mabao 2-0 katika mechi ya Europa Cup.

  Genk iliyokuwa nyumbani, ilipata bao katika kila kipindi huku Mtanzania akiingia katika kipindi cha pili, ilikuwa dakika ya 56 na kuchangia kupatikana kwa bao la pili.

  Bao la kwanza lilifungwa na Jakub Brabec aliyeunganisha pasi safi ya Leon Bailey katika dakika ya 40, wakaenda mapumziko wakiwa wanaongoza.

  Samatta aliingia kuchukua nafasi ya Thomas Buffel katika dakika ya 56 na kaanza kuonyesha cheche.

  Dakika ya 83, Onyinye Ndindi alifunga bao la pili na kushindilia msumari wa mwisho kwa Wahispania hao.


  Bilbao ni kati ya timu zenye historia ya juu katika La Liga kwa kuwa ni kongwe na haijawahi kuteremka daraja kutoka La Liga. Nyingine ambazo hazijawahi kuteremka ni Real Madrid na Barcelona tu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SAMATTA ATOKEA BENCHI NA KUISAIDIA GENK KUITWANGA BILBAO MABAO 2-0 EUROPA CUP Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top