Header Ads

Siri Za Chumbani Za Uwoya, Wolper Zaanikwa!

Irene_Uwoya028  Staa wa Bongo mwenye mvuto, Irene Uwoya.
Stori: Hamida Hassan, Ijumaa
Mastaa wa kike wenye mvuto Bongo, Irene Uwoya na Jacqueline Wolper wamezungumza na gazeti hili na kwa mara ya kwanza wameamua kuanika siri zao za chumbani ambazo wanadai ndizo zinazowafanya wajione ni wanawake waliokamilika.
wolper Staa wa Bongo mwenye mvuto, Jacqueline Wolper.
Wakizungumza na paparazi wetu kwa nyakati tofauti, mastaa hao walisema kuwa, wameamua kufanya hivyo ili mashabiki wao wawajue kinagaubaga kuhusiana na fani yao lakini pia maisha yao ya kimapenzi.
Katika mahojiano hayo, wa kwanza kufunguka alikuwa ni Wolper na mahojiano kati ya Ijumaa na yeye yalikuwa kama ifuatavyo;
Ijumaa: Ni lipi unajivunia unapokuwa faragha?
Wolper: Mwanamke siku zote unatakiwa kuwa mtundu na mbunifu, kinyume na hapo lazima utaibiwa.
Ijumaa: Je, ukiwa chumbani unapenda kuvaa nguo gani? Namaanisha rangi na fasheni ya nguo.
Wolper: Napendelea sana vigauni vifupi ‘transparent’, hasa rangi ya pinki.
Ijumaa: Unapokuwa na mtu wako, unajisikia poa akiwa amevaa mavazi gani?
Irene_Uwoya004 Irene Uwoya akiwa katika pozi.
Wolper: Hee, avae tena? Kama ni suala la kuvaa basi avae nguo zangu za ndani, hapo itakuwa poa.
Ijumaa: Kitu gani muhimu ambacho huwezi kukikosa uwapo faragha na mtu wako?
Wolper: Kwanza manukato lazima yahusike sana, si unajua mwanamke kunukia? Halafu mambo ya ‘kachumbari’ kwa sana.
Ijumaa: Kachumbari ndiyo nini?
Wolper: Hayo ni mambo ya wakubwa bwana, kama hujaelewa tuache.
Ijumaa: Manukato gani huwa unatumia ukiwa chumbani?
Wolper: Kwa kweli ni udi maana manukato yake yanafiti sana eneo hilo.
wolper (1) Jacqueline Wolper akiwa katika pozi.
Baada ya Wolper kufunguka hayo, Uwoya naye alitafutwa ambapo naye aliweka wazi baadhi ya mambo yake ya chumbani huku mengine akidai ni siri yake na baby wake.
Ijumaa: Chumba chako hasa ukiwa na baby wako huwa kinapambwa na mashuka ya rangi gani?
Uwoya: Mimi ni msafi sana linapokuja suala la chumba changu, ndiyo maana napendelea mashuka meupe ili uchafu ukiingia kidogo tu niuone.
Ijumaa: Kwa upande wa mavazi huwa unapendelea kuvaa nguo gani pale baby wako anapokuwa pembeni yako?
Uwoya: Ni kanga moja tu, si unajua eneo hilo wala huhitaji kujivika minguo?
Ijumaa: Sawa, manukato unayotumia je?
Uwoya: Huwezi kuamini napendelea pafyum za kiume sana na hizo ndizo hujipuliza nikiwa chumbani na mtu wangu.
Ijumaa: Kipi ambacho ukifanyiwa na mpenzi wako unajisikia furaha?
Uwoya: Kikubwa napenda sana utani, tutaniane sana! Lakini pia napenda sana kudeka.
Hata hivyo, kwa Uwoya yapo maswali ambayo aliomba asiyajibu kwa kuwa kimaadili ya Kibongo siyo sahihi.

No comments