• Latest News

  October 31, 2016

  Ukweli wa Miss Tanzania 2016/2017, Diana Edward Loy, Ajawahi Kujiunga na Chuo

   

  TAARIFA KWA UMMA

  Napenda kuujulisha Umma yafuatayo;

  1. Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshinda taji jana jijini Mwanza, anaitwa Diana Edward Loy na siyo Diana Lukumai kama inavyotajwa mitandaoni.

  2. Mlimbwende huyo amemaliza kidato cha nne 2015 Shule ya Sekondari Arusha Day na si 2011 kama inavyotajwa mitandaoni kwa malengo ovu.

  3. Diana hajawahi kujiunga na Elimu ya Chuo Kikuu chochote Tanzania au duniani bali anatarajia kujiunga mwaka huu katika chuo cha IFM kusomea masula ya kodi ngazi ya stashahada (cheti) ingawa kulingana na ratiba zake na majukumu yake mapya ikiwemo kushiriki Miss world mapya huenda akaahirisha mwaka wake wa masomo.

  4. Tunawasihi watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii na si kufanya "Character assassination" lakini pia tunaheshimu haki yao ya msingi ya kuhoji masuala ya msingi kabisa kuhusu mtu ambaye ni Public figure na ataliwakilisha taifa katika anga za kimataifa.

  Tumuunge mkono mlimbwende wetu ili atuletee Taji la Dunia.

  Ahsanteni.

  Charles William
  Kaimu Ofisa Habari wake.
  0716719589 (wilflow101@gmail.com). CnP

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Ukweli wa Miss Tanzania 2016/2017, Diana Edward Loy, Ajawahi Kujiunga na Chuo Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top