Header Ads

Video Moyo Mashine Ya Ben Pol Ina VijidosariNA WASTARA JUMA
NI siku nyingine tena tunakutana katika kona yetu hii ya Movie and Video Review (Uchambuzi wa Filamu na Video za Kibongo).
Baada ya wiki iliyopita kwenye kona hii kuwepo kwa Dairekta Haji Adam ‘Baba haji’ leo nitakuwepo mwenyewe dairekta wa filamu Bongo, Wastara Juma.
   

Leo ningependa kuichambua video ya mwanamuziki wa Bongo Fleva anayefahamika kama Bernard Paul ama wengi wamezoea kumuita Ben Pol.
Ni moja kati ya video alizozifanyia nchini Afrika Kusini chini ya Dairekta Nick ambaye pia aliyewahi kuzitengeneza video nyingi za Bongo ikiwemo Salome ya Diamond pamoja na Bado ya Harmonize.


UZURI
Kwa upande wa audio, nisiwe mnafiki audio imesukwa vizuri, ni nzuri inagonga ngome za masikio vilivyo. Ni moja ya wimbo ambao si mtoto wala mtu mzima akiusikia hata mara moja lazima atanasa baadhi ya mistari.
VIDEO QUEEN KACHE-MKA
Nime-jaribu kuiangalia mara nyingi hii video huku nikimfuatilia video queen aliyetumika lakini nimeona kuwa hana ubunifu. Katika video hii nguo aliovaa ni moja mwanzo mwisho wakati kwa upande wa Ben Pol ameba-dilisha zaidi ya mara mbili. Si mbaya sana alivyo-fanya lakini kwa video queen kuwa na nguo moja mwanzo mwisho hilo nalo linamkera mtazamaji.


UCHACHE WA WAHUSIKA
Asilimia kubwa ya video hii imetawaliwa na wahusika wawili tu yaani Ben Pol na video queen wake. Kuna sehemu moja tu tena inaonekana katikati wakiwa mezani na wawili wengine kama wanawafuata. Ushauri sehemu nyingi zilipaswa kuwa na wahusika angalau watatu-wanne kuiongozea mvuto.

KINANDA KINACHOCHOMWA
Nimejiuliza mara nyingi kuhusiana na kinanda kilicho-tumika katika video hii na yalioimbwa. Hakuna ‘connection’ yoyote. Sijajua umu-himu wa kutumia kinanda kikiwa kinach-omwa moto. Mfano video imeanza tu kinanda kinaungua, sehemu nyingine mtu akikipiga kinanda hichochicho na mwishoni kinanda kikimalizika kuteketea. Mtazamaji unamuacha njia panda, angalau basi Ben Pol angekuwa ndiyo anakipiga kile kinanda huku anamuimbia yule video queen kidogo kingeleta connection.

USH-AURI
Wakati mwin-gine si kuki-mbilia nje ya nchi kutoa video yenye mazingira kama ya nyumbani. Ni wazi video hii ingechukuliwa mazingira ya huku ambayo yanafanana pengine kuzidi hata ya huko, ingetoka zaidi ya bomba.

No comments