Header Ads

Vyakula 10 vinavyoongeza Nguvu Za Kiume!

BAADA ya wiki iliyopita kuzungumzia vyakula kwa wagonjwa wa kisukari, wiki hii tutaeleza vyakula kwa wanaume wenye tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Ukweli ni kwamba upungufu wa nguvu za kiume hauondolewi kwa dawa za kuchochea nguvu wakati wa tendo.


 Hizi zina madhara makubwa na mara kadhaa husababisha vifo kwa wanaume  kwani hulipua moyo. Ni lazima kiini cha tatizo hili kichunguzwe na tiba stahiki ipatikane. 

Kinyume cha hapo, janga hili linaweza kugeuka na kuwa balaa kubwa katika jamii. Matatizo ya nguvu za kiume huchangiwa na kuugua kwa muda mrefu, ugonjwa wa kisukari, kuvaa nguo za kubana sana na mengineyo. 

Pia dawa za kuua wadudu huleta tatizo hili kwani zina viambata sumu viitwavyo ‘estrogen’, matatizo ya kisaikolojia, kujichua kwa muda mrefu na kutumia vyakula vyenye kemikali. Utafiti unasema kuna uhusiano mkubwa kati ya upungufu wa nguvu za kiume na kuwa na sumu mwilini zinazotokana na vyakula vyenye kemikali tunavyokula.Kuna aina 2 ya vyakula ambavyo vimefanyiwa utafiti na kubaini kuwa ni moja ya vyakula vinavyosaidia kuongeza nguvu za kiume na havina madhara. Vyakula hivyo vyenye uwezo wa kuongeza nguvu za kiume kiasili ni:

 MBEGU ZA MABOGA
 Ziloweke katika maji yenye chumvi, zikaushe. Zikaange kidogo bila kuziunguza. Tafuna mbegu 100 kutwa mara tatu kwa muda wa mwezi mmoja. Ukitafuna meza vyote na makapi yake. Mbegu hizi sifa yake kubwa ni kuongeza wingi wa mbegu za kiume (manii), kama unatatizo la kuwa unatoa manii machache (low sperm count) basi hii ni muhimu sana kwako.  

CHAI YA TANGAWIZI 
Tangawizi ni kinywaji ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini na zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi.

 

Inaweza kuliwa mbichi, au kupika au kuanikwa na kuwa kama unga. Ulaji wa tangawizi mbichi nusu saa kabla ya tendo la ndoa husaidia katika kuongeza hamu na nguvu ya tendo la ndoa. 

Unaweza ukanywa chai ya tangawizi tu nusu saa kabla ya kuanza tendo au unaweza ukatafuna kipande cha tangawizi mbichi kwa ukubwa wa dole gumba la mtu mzima nusu saa kabla ya tendo. Kunywa chai ya tangawizi mbichi kila siku, katika chai hiyo unayopika ndani yake weka tu maji na tangawizi mbichi uliyosagia ndani yake (usiongeze majani ya chai humo), kumbuka tangawizi inaoshwa tu na maji na uisagie ndani ya sufuria pamoja na ganda lake la nje. 

Sasa badala ya kutumia sukari wewe tumia asali kwenye hii chai yako ya tangawizi na ukiitumia hivi kila siku hutachelewa kuona faida zake. Tangawizi peke yake ni dawa ya asili mwilini! 

KITUNGUU SWAUMU Chukua punje nane mpaka 10 za kitunguu swaumu, menya na uzikate vipande vidogo vidogo kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 2 kwa mwezi mmoja. Pia hakikisha kila chakula unachopika basi kitunguu swaumu lazima kiwemo kama moja ya viungo na ukiweke mwishoni mwishoni kwamba kisiive sana katika moto wakati unapika chakula.   

TIKITIMAJI Chakula kingine kinachosaidia katika upande wa kuongeza nguvu za kiume ni tunda la tikitimaji, unaweza ukachukua tikiti lako ukalikata na kutengeneza juisi kisha
unakunywa ila siyo lazima utengeneze juisi hata lenyewe tu unaweza ukalila. Ila jitahidi kutumia tunda hili kila siku kwani linasaidia sana kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume. 


PARACHICHI Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali wa kimapenzi na kwa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana. 

UGALI WA DONA Kula ugali wa dona kila siku. Ni muhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na muhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukua mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote. 

ASALI NA MDALASINI Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 4 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja 

NDIZI. Ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.  

MVINYO MWEKUNDU 
Mvinyo mwekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa. 

CHAZA NA PWEZA 
Aina hizi za samaki huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalishaji wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.

No comments