Header Ads

Amber Lulu, Lulu Diva kupendezesha Usiku wa Mastaa Leo Maisha Basement

VIDEO Queen wanaotikisa kunako video za Kibongo kwa sasa, Lulu Auggen ‘Amber Lulu’, Lulu Abass ‘Lulu Diva’ na wengine kibao wanatarajiwa kutikisa katika Usiku wa Mastaa utakaofanyika Jumapili hii ndani ya Ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama jijini Dar.

 
Akizungumza na Showbiz, mratibu wa shoo hiyo, Geoffrey Jilla ‘Jilla the Boss’ alisema kuwa, mbali na uwepo wa video queens hao, mashabiki wa burudani wategemee kupiga picha ‘red carpet’ na kukata keki na mastaa mbalimbali wa filamu na muziki Bongo.

“Shoo hii pia itawapa fursa wale wote waliozaliwa Novemba 11 kukata keki pamoja na mastaa mbalimbali. Tutakuwa na burudani kutoka kwa wakali kibao wa Bongo Fleva wakiongozwa na Mesen Selekta, Country Boy, Bob Junior, Pam D na wengine kibao kwa mtonyo wa 10,000 tu,” alisema Jilla.

No comments