Header Ads

Aunt Ezekiel Ateketeza Laki Sita Kwa Picha (Zicheki Hapa)H
IVI karibuni kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na Instagram, habari ya mjini ilikuwa ni staa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel (28), pamoja na mzazi mwenzie Moses Iyobo (22), kutokana na picha zao mbalimbali walizokuwa wamezitupia wakiwa pamoja na mtoto wao, Cookie.
Staa huyo aliyeolewa na mfanyabishara Sunday Demonte kisha jamaa huyo kufungwa kwa msala wa madawa ya kulevya Uarabuni,  baadaye Aunt alimkabidhi Iyobo moyo wake na kufanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja.
Katika kuelekea siku ambayo Aunt amezaliwa, Oktoba 27, mwigizaji huyo na familia yake hiyo mpya walijifotoa picha zaidi ya 30 kisha kuziposti mtandaoni.
Anazungumziaje picha hizo?
“Unajua mimi kama mimi kwanza kabisa napenda sana kupiga picha lakini pamoja na hayo kikubwa zaidi  nimefanya vile kwa ajili ya familia yangu na kuweka kumbukumbu yangu ya uzeeni sasa kama kuna watu wengine wanaziongelea tofauti ni mitazamo yao.

Ametumia fedha kiasi gani kupiga picha hizo?
“Katika picha hizo nimetumia kama laki sita kwa sababu nilizipiga kwa awamu tatu tofauti, mavazi tofauti ambapo kila awamu ni kiasi cha shilingi laki mbili na nilipiga ikiwa ni karibu na siku yangu ya kuzaliwa. Naziachia taratibu mitandaoni kuna nyingine bado sijaziachia mpaka sasa.

Wakitibuana
na Iyobo itaKUwaje?
“Kwanza kwa nini nitibuane na mtu ambaye nampenda kwa moyo wangu wote hilo halipo na kama siku likitokea siwezi kufuta hizo picha kwa sababu hiyo pia ni kumbukumbu kwa mtoto wangu kwa baba yake.

Vipi kuhusu
kumpita umri Iyobo
“Sijaona tatizo lolote hapo, mbona wadada wadogo wanatoka kimapenzi na mijibaba iliyowapita umri kabisa tena miaka ishirini mbele sembuse mimi na Iyobo wangu, kwanza hayo ndiyo mapenzi mazuri asikwambie mtu.

Akiolewa tena,
atafanya sherehe?
“Tena sherehe yenyewe siyo ya mchezomchezo, kwa nini nisifanye sherehe kwa mtu ambaye amegeuza maisha yangu na kunifanya niitwe mama na kupata heshima kama mwanamke? Mpunga lazima uliwe na watu waserebuke sana tu.

Ana mpango wa
kuzaa tena na Iyobo?
“Muda si mrefu linafanyika hilo kwa sababu tumeshakaa na kupanga tukaona ni bora kufanya hivyo  mapema kwa sababu tuna muda tumejiwekea wa kufanya mambo ya kazi na si kuzaa tena hivyo tumeona bora tumalize hiyo kazi kabisa. 

Sanaa imempa nini
katika maisha  yake?
“Sanaa imenifanyia kitu kikubwa sana maishani mwangu, sasa hivi niko mbioni kumaliza nyumba yangu.

Anakumbuka kitu
gani kwa Kanumba?
“Yule jamaa siwezi kumsahau maisha yangu yote ni mtu ambaye amefanya mpaka wengine kuwepo hapa tulipo leo. Ana mchango mkubwa sana kwangu na wengine wengi.

Anasemaje kukwama soko la filamu?
“Hakuna zaidi ya wasambazaji kwa sababu kulikuwa na mtu mmoja tu ambaye anaaminika naye tena akawa haendi sawa kama zamani kwa hiyo sasa vitu vinakuwa siyo kama zamani na wasanii wamesambaratika,” alimaliza Aunt.

Msikie Iyobo juu ya
penzi lake kwa Aunt
“Kuna watu wengi sana nasikia wanazungumzia kuhusu  umri wangu ni mdogo sasa ni hivi sijaona ukubwa wa mpenzi wangu namuona bado mtoto mdogo mimi pia nafurahi kuwa na mpenzi ambaye amenipita kama alivyo yeye kwa sababu mapenzi yake yana ladha tofauti kabisa.”

No comments