Header Ads

Breaking News: Ndege Iliyobeba wachezaji wa klabu ya Chapecoense wa Brazil Yaanguka Colombia

Kabla ya kuanza safari timu hiyo ilipiga selfie hii.

NDEGE iliyokuwa imebeba watu 72, ikiwemo timu ya soka ya klabu ya Chapecoense ya Brazil imeanguka katika sehemu ya milima nchini Colombia  wakati inakaribia Mji wa Medellin.
Maelezo kamili ya ajali hiyo hayajafahamika lakini habari zinasema kwamba kuna watu walionusurika.

Ndege hiyo ya kukodisha iliyokuwa ikitokea Bolivia, ilikuwa na timu ya  soka ambayo ilikuwa icheze katika fainali ya Kombe la Amerika ya Kusini dhidi ya timu ya Atletico Nacional ya Medellin.  Hivyo, fainali hiyo imeahirishwa.

Ripoti zinasema ndege hiyo yenye leseni namba CP 2933, iliyoanguka muda mfupi kabla ya saa sita usiku, ilielezewa na Meya wa Medellin, Federico Gutierrez, kama “janga kubwa”, akiongeza kwamba  inawezekana kuna watu walionusurika.
Mabaki ya ndege iliyoanguka.

Mmoja wa wachezaji wa klabu ya Chapecoense, Alan Ruschel (27) akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kutolewa kwenye ndege hiyo.
Ndege iliyoanguka.
Wachezaji wa klabu ya Chapecoense

No comments