Header Ads

CALISAH; WEMA AMEKUPA FUNZO, SIMAMA SASA!

NIMELAZIMIKA kukuandikia barua, Modo Ibrahim Mgimbu ‘Calisah’. Si bure sababu nimeona una kipaji, unajua kujieleza  na penginne unaweza kuwabadilisha vijana wengi tu kupitia tasnia hiyo ya umodo.
Nimeona matangazo yako mbalimbali na baadhi ya video ambazo umetokea. Inaashiria kwamba kazi hiyo ukiifanya kwa moyo, juhudi na maarifa, unaweza kuendesha maisha yako na maisha yakaendelea mjini.Nimekufuatilia kupitia mjadala wa hivi karibuni kuhusu suala lako na Wema. Nimegundua kwamba, kwanza wewe na Wema mlikuwa mkishirikiana kwa muda mrefu katika masuala ya kisanii. Ni ile ‘win- win situation’. Kwa namna moja au nyingine yeye alikuwa akipata kitu kutoka kwako na wewe kuna vitu ulikuwa unafaidi kutoka kwake.Kama hiyo haitoshi, nimejifunza kwamba ulikuwa kwenye uhusiano wa siri na Wema. Wewe mwenyewe kupitia mazungumzo yako na Global Publishers, ulionesha dhahiri kwamba aina ya uhusiano wa siri ndiyo staili uipendayo maishani.
Hivyo mlikutana na Madam, mkapendana na mkafanya hayo mliyoyafanya kwa siri. Mliamua kufanya siri kwa ajili ya ‘afya’ ya makubaliano yenu mliyoyajua wenyewe. Si wewe, si Madam. Hakuna hata mmoja kati yenu aliyekuwa wazi kuanika penzi lenu.
Kila aliyekuwa akihojiwa kwenye vyombo vya habari, alikanusha kuhusu suala la uhusiano. Zaidi mlilitanguliza lile la ‘project’ za kikazi.


Hata ile video, haikuwa dhamira yenu kuvuja. Pengine mlipendelea kucheza vizuri sinema yenu ili pale mtakapokuja kumwagana mtu asijue. Aina hiyo ya uhusiano huwa mara nyingi huwa na tafsiri ya kupeana mwanya wa kila mtu kuweza kuwa ‘michepuko’ halafu mkirudi nyumbani mnaendeleza penzi lenu.
Rafiki yangu Calisah, unajua mwenzako nilienda mbali sana kimawazo. Kuna wakati niliwahi kuwaza pengine kipindi ambacho wewe ndio penzi lebu motomoto, labda Madam alikuwa akiandika kwenye magazeti kwamba anatembea na mtu mwingine.
Yani wewe ulikuwepo lakini aliyekuwa anaonekana kwenye vyombo vya habari ni mwingine tofauti. Sijui alikuwa Diamond? Sijui alikuwa ni Idris Sultan? Siishangai sana hiyo maana najua mara nyingi uhusiano wa siri huwa unatoa mwanya mzuri tu wa kila mmoja kuwa na matawi mengine.
Lakini dhumuni la kukuandikia barua hii, nilitaka kukueleza kwamba suala hilo liwe ni funzo kwako. Umegundua kwamba ulikuwa kwenye uhusiano wa namna gani. Aliyekupa simu kwa mapenzi yake, ndiyo  huyo huyo aliyekuja kukunyang’anya pale alipoihitaji.


Ndiye aliyekusababishia watu wakushambulie kwamba ulikuwa unalelewa na Madam. Amekufanya uonekane wewe ni mtu wa kuhongwa, wakakupigia kelele sana kwamba hata gari alikuhonga japo mwenyewe ulifafanua kwamba lilikuwa la kwako.
Usikubali kunyanyasika eti kwa kuwa tu una kitu unakitaka kwa mtu fulani. Wewe kipaji unacho, unayo nafasi ya kufanya shuguli zako mwenyewe, pambana na utafanikiwa. Mtoto wa kiume, hutakiwi kulalamika kwamba wapambe wa Wema ndio wamechangia kwa kiasi kikubwa wewe kugombana naye, kwa nini usichane nae?
Mimi nakushauri, fanya maisha yako.  Pambana na matangazo, ikiwezeekana igiza sinema maana muonekano wa kuigiza unao, utafanikiwa!
Nakutakia mafanikio  mema, mimi ni rafiki yako;

No comments